Pages

January 10, 2015

MWANABLOG APATA KIPIGO KIKALI KWA KUKASHIFU DINI

http://www.sienteamerica.com/media/cache/a7/f9/a7f98da7b7f95aefc282610419007611.jpg
Mwanablogu wa Saudi Arabia akichapwa viboko ikiwa sehemu ya hukumu iliyopo ndani ya kifungo cha miaka 10 jela.
Mwanablogu nchini Saudia amechapwa viboko hadharani kwa madai ya kutusi dini ya kiislamu.

Raif Badawi ambaye alianzisha mtandao kwa jina ''Liberal Saudi Network'' alihukumiwa kifungo cha miaka 10 msimu wa joto uliopita.

Mahakama pia iliagiza acharazwe viboko 1000.
Amechapwa viboko hivyo katika mji wa Jeddah.

Ilieleweka kwamba angetandikwa viboko hamsini na kwamba alitarajiwa kuchapwa viboko zaidi wiki zilizofuatia.

Mwanablogu huyo alichapwa viboko licha ya wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani kutaka kuondolewa kwa adhabu hiyo walioitaja kama ya kikatili.BBC

No comments:

Post a Comment