Pages

January 8, 2015

Maisha yalikuwa magumu, akambeba mbwa na kumtelekeza kituo cha treni

DOG 1
Mbwa na paka ni wanyama ambao wanafugwa na watu wengi na majumbani, ni wachache ambao wanapata matunzo mazuri lakini kwa huku kwetu wengi huwa wazururaji mitaani.
Mbwa huyo  aina ya shar-pei amekutwa  akiwa amefungwa kamba shingoni  kwenye chuma kimoja ndani ya kituo hicho, huku pembeni yake kukiwa na  begi ambalo ndani yake kulikuwa na mto wa kulalia wa mbwa huyo, kifaa chake cha kuchezea, bakuli la chakula, na chakula chake, pamoja na namba za  simu za mtu ambaye alikuwa akimfuga.
DOG2Mkaguzi wa kituo hicho cha treni Stewart Taylor amesema walipowasiliana na mmiliki wa mbwa huyo, amesema alimuuza tangu mwaka 2013 lakini hakuwa na kumbukumbu juu ya mteja waliyemuuzia, Shirika la kutetea Haki za Wanyama limesema kitendo hicho ni cha kikatili na wanamtafuta mhusika ili awajibishwe.
Japo haiko wazi sababu ilimfanya mwenye mbwa huyo amtelekeze mbwa wake, wengi wanahisi huenda ni gharama kubwa za matunzo kwa mbwa huyo.

No comments:

Post a Comment