Mbwa na paka ni wanyama ambao wanafugwa na watu wengi na majumbani, ni wachache ambao wanapata matunzo mazuri lakini kwa huku kwetu wengi huwa wazururaji mitaani.
Mbwa huyo aina ya shar-pei amekutwa akiwa amefungwa kamba shingoni kwenye chuma kimoja ndani ya kituo hicho, huku pembeni yake kukiwa na begi ambalo ndani yake kulikuwa na mto wa kulalia wa mbwa huyo, kifaa chake cha kuchezea, bakuli la chakula, na chakula chake, pamoja na namba za simu za mtu ambaye alikuwa akimfuga.
Mkaguzi wa kituo hicho cha treni Stewart Taylor amesema walipowasiliana na mmiliki wa mbwa huyo, amesema alimuuza tangu mwaka 2013 lakini hakuwa na kumbukumbu juu ya mteja waliyemuuzia, Shirika la kutetea Haki za Wanyama limesema kitendo hicho ni cha kikatili na wanamtafuta mhusika ili awajibishwe.
Japo haiko wazi sababu ilimfanya mwenye mbwa huyo amtelekeze mbwa wake, wengi wanahisi huenda ni gharama kubwa za matunzo kwa mbwa huyo.
No comments:
Post a Comment