Na Habiba Yahya, Morogoro.Mvua kubwa iliyodumu kwa takribani saa moja na nusu mjini Morogoro jana, imeathiri miundombinu ya barabara na shughuli mbalimbali zikiwamo huduma za kijamii na biashara, kusimama.
Mvua hiyo
iliyoanza kunyesha saa 5 asubuhi hadi
saa 6: 30 mchana, ilisababisha barabara za mitaa kadhaa ya katikati ya mji wa
Morogoro kufurika kwa maji.
Hali hiyo
iliathiri usafiri hasa kwa watu wanaotumia pikipiki maarufu kama bodaboda.
Barabara zilizoathirika zaidi ni pamoja na ile
ya Kihonda kwenda katikati ya mjini na Barabara ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
kwenda Stendi ya Daladala.
Lakini pia
eneo la stendi hiyo pia lilifurika kwa maji ambayo baadaye waliingia ndani ya
magari.
Daladala
zinazotoa huduma kati ya stendi hiyo na maeneo ya Sua, Mazimbu na Kihonda zililazimika kusitisha
shughuli za usafirishaji kwa muda kwa sababu barabara zilikuwa zimekufurika kwa
maji na baadaye foleni kubwa.
Katika eneo
la Kikundi ambako kuna mkondo wa
maji, huduma za usafiri zilisimama baada ya wenye mgari kuhofia magari yao
kusombwa
Mvua pia
imesababisha kuvunjika kwa kuta za daraja lililopo katika Barabara ya Ahmadiya
kuelekea Mtaa wa Ngoto.
.
Pamoja na
mvua hiyo kuathiri shughuli mbalimbali
lakini ilikuwa neema kwa wauza miamvuli ambao walitumia fursa hiyo kufanya
biashara yao mitaani.
Miamvuli
hiyo ilikuzwa inauzwa kwa bei ya juu ikilinganishwa bei ya kawaida katika siku
ambazo hazina mvua.
Mwamvuli
mdogo ulikuwa ukiuzwa kwa bei ya kati ya Sh5,000 na Sh6,000 wakati kwa bei ya
kawaida unauzwa kwa bei ya kati ya Sh2,500 Sh 3,000.
Miamvuli
mikubwa ilikuwa inauzwa kwa bei ya kati ya Sh7, 000 na Sh8000 lakini bei yake
ya kawaida ni kati ya Sh 4,000 na Sh 5,000.
No comments:
Post a Comment