Pages

January 14, 2015

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AMPANDISHA CHEO CHA SAJIN WA MAGEREZA ASKARI WA KIKE, MWANARIADHA WA KIMATAIFA JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimvisha cheo cha Sajin wa Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa, CPL. Catherina Lange(hivi sasa cheo cha sajin) wa Gereza Kuu Arusha ambaye ambaye hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla. hafla hiyo imefanyika leo Januari 13, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza Sajin wa Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa, wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla rasmi ya kumvalisha cheo hicho ambapo askari huyo hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(Meza kuu) akitoa maelezo mafupi kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) namna Askari Mwanariadha wa Kimataifa, CPL. Catherina Lange(hivi sasa cheo cha sajin) wa Gereza Kuu Arusha alivyoshiriki kwa mafanikio makubwa katika mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
Wanahabari toka Vyombo mbalimbali vya Habari wakifanya mahojiano Maalum na Askari Mwanariadha wa Kimataifa, Sajin wa Magereza Catherina Lange(hayupo pichani) wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe akimpa pongezi Askari Mwanariadha wa Kimataifa, Sajin wa Magereza Catherina Lange(kulia) wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hamis Nkubas akiwa katika picha ya pamoja na Askari Mwanariadha wa Kimataifa, Sajin wa Magereza Catherina Lange(katikati) wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Kuu Arusha, Themistocles Ifunya.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment