Pages

January 5, 2015

Hii haikuwa taarifa nzuri kwa walaji wa mikate Nigeria…


Freshly Baked Cinnamon Muffins 
Wengi wetu ni wapenzi wa vitafunwa, maandazi, keki, mikate ni baadhi tu ya vile ambavyo tumezoea kuvitumia majumbani kwetu kwa ajili ya kifungua kinywa.

Kuna wakati mwingine hatujui vitafunwa hivi vinaandaliwa katika mazingira gani.
Kutoka Nigeria jimbo la Delta hii imeshtua wengi, ni mama mmoja kukubali kosa kwamba amekuwa akitumia mkojo kuandaa keki akitumia ambazo ni maarufu kwa jina la moi-moi, inahusishwa na imani za kishirikina.

Jina maarufu la mama huyo anaitwamama T alikiri kufanya kosa hilo baada ya kupigwa na watu wenye hasira.

Jamaa ambaye ni mmoja ya watu walishuhudia tukio hilo amesema alikuwa anaoga, ghafla akatokea panya aliyetaka kumuuma mguu, akampiga na mti panya akafa, muda mfupi baadaye panya aliongezeka ukubwa na baadaye kuwa mtu halafu akakimbia akiwa amevaa kandambili moja na moja akaiacha.

Alipotoka ili akasimulie wenzake alikuta kundi la watu waliomzunguka mama huyo akiwa amevaa kandambili moja mguuni.

Baada ya ushahidi huo walimpiga akakubali kufanya vitendo vya kishirikina na pia kutengeneza mikate hiyo ambayo inaitwa ‘moi-moi’ akitumia mkojo.
moinmoin
Jinsi ambavyo mikate hiyo ya asili inaandaliwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...