MICHUANO
ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2015 imeanza kutimua vumbi nchini Guinea ya
Ikweta kwa mechi mbili za kundi A kupigwa siku ya ufunguzi.
Mechi
ya kwanza iliyoanza majira ya saa 1:00 usiku jana, wenyeji Guinea ya
Ikweta walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Congo Brazaville.
Guinea
ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 17 kupitia kwa
Emilio Nsue, lakini Congo walisawazisha dakika ya 87’ kupitia Thievy
Bifouma.
Mechi ya pili iliyomalizika iliyoanza saa 4:00 usiku, Gabon walipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Burkina Faso.
Mabao ya Gabon yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang katika dakika ya 19 na Malick Evouna katika dakika ya 72.
Kwa matokeo hayo, Gabon wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 3 ambapo wamecheza mechi moja, wameshinda moja na hawajafungwa.
Nafasi ya pili inashikwa na Gabon wanaofanana kwa kila kitu na Congo Brazaville katika nafasi ya tatu.
Wote wamecheza mechi moja, wametoa sare moja, wamefungana goli moja moja.
Burkina Faso wanaburuza mkia katika kundi A baada ya kufungwa mechi yao ya kwanza usiku huu.
No comments:
Post a Comment