Pages

January 13, 2015

DUKA LA ZURII HOUSE OF BEAUTY LAFUNGULIWA RASMI NDANI YA DAR FREE MARKET JIJINI DAR

Na Mwandishi  Wetu
MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige  leo amezindua rasmi  duka  jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi  Jijini Dar es Salaam.

Akizindua duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza  nyumbani hali ambayo imeweza kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.

“Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza  Jestina  kwani ameonesha  mfano  wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa  kwa wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.

Aidha alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine  pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.

Wakati huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina  alisema kwamba yeye ameona  fursa za  kuwekeza nyumbani  hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.

“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu  fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru  Mungu kwa kutimiza ndoto hii”.     
 Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige  akikata utepe katika ufunguzi wa ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi lililofunguliwa rasmi leo Jumatatu 12 Jan 2015  kulia ni Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George. 
 Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akifungua duka rasmi 
   Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George  akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige kuhusu bidhaa zilizopo kwenye duka la ZuRii Fashion & Beauty Boutique
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akizungumza na vyombo vya habari kwenye ufunguzi wa duka hilo la vipodozi
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika kufanya manunuzi ndani ya duka hilo
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George( kulia) akiwa na mwana harakati mwenzake Shamim Mwasha mmiliki wa blog ya 8020.
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kuhusu ufunguzi na ujio wa duka hilo hapa nchini Tanzania likiwa na muonekano tofauti
 Mmoja wa wateja waliofika katika duka hilo akitizama bidhaa


Muonekano wa duka la Zurii kwa ndani

No comments:

Post a Comment