Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon pamoja na washiriki wa hafla ya
kuwakumbuka walinzi wa amani wakisimama kwa dakika moja kuwaenzi walinzi
wa amani na watoa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi wa umoja
wa mataifa waliopoteza maisha wakati wa tetemeko kubwa la ardhi
lililotokea nchini Haiti mwaka 2010 na wale ambao wamepoteza maisha kati
ya Octoba 2013 na Novemba 2014.
Ban Ki
Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambayo iliibua hisia na majonzi
makubwa miongoni wa washiriki wa hafla hiyo ya kuwaenzi walinzi wa amani
na watoa misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza
wajibu wao wa kuwasaidia wananchi waliokuwa matatizoni. Miongoni mwa
wahanga hao waliokumbukwa katika hafla hiyo ni Mashuja Watatu Kutoka
Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) waliopoteza maisha wakati
wakitimiza wajibu wao katika Misheni ya Kulinda Amani ya MONUSCO katika
Jamhuri ya Kidemokraria ya Kongo. Mashujaa hao ni Luteni Rajabu Mlima,
Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila
Mwakilishi
wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
Balozi Tuvako Manongi akitoa heshima zake mbele ya mshumaa mkubwa ambao
uliandaliwa kama ishara ya kuwakumbuka na kuwaenzi Walinzi wa Amani na
Watoa Misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza
majukumu yao katika kipindi cha tetemeko la aridhi lililotokea mwaka
2010 huko Haiti na wale waliopoteza maisha kati ya Octoba 2013 na
Novemba 2014. katika kipindi hicho Tanzania ilipoteza mashujaa wake
watatu waliokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO huko DRC
Na Mwandishi Maalum
Umoja wa
Mataifa jana Alhamisi umewakumbuka walinzi wa Amani na wafanyakazi ya
umoja wa mataifa waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yako
katika kipindi cha Octoba 2013 na November 2014.
Kumbukumbuka
hiyo imefanyika katika siku kama ya jana ( January 8) miaka mitano
iliyopita palitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti na kupoteza
maisha ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo pamoja na uhalibifu mkubwa
wa mali ilivuta hisia za waliohudhuria hata baadhi yao kutokwa na
machozi
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akizungumza katika hafla hiyo
amesema, anasikitishwa sana na ongezeko la mashambulizi yanayofanywa
dhidi ya walinzi wa Amani pamoja na watoaji wa misaada ya kibinadamu
ambao ni wafanyakazi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
Jumla ya
wahanga 102 walipoteza maisha nchi Haiti wakati lilipotokea tetemeko
hilo mwaka 2010, huku wengine 100 walipoteza maisha kati ya Octoba 2013
na Novemba 2014. Wahanga hao ni walinzi wa Amani na wafanyakazi wa
Umoja wa Mataifa kutoka mataifa mbalimbali duniani na walikuwa
wakihudumu katika Misheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa na Mashirika
yake.
Kati ya
waliokumbukwa jana wapo walinzi wa Amani watatu kutoka Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambao walipoteza maisha huko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo walikokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO.
Mashujaa
hao wa kitanzania na ambao majina yao yalisomwa moja baada ya jingine
sambamba na mashujaa wenzao wengine. Ni Luteni Rajabu Mlima, Private
Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila.
Ban Ki
Moon amesema walinzi wa Amani na watoaji wa misaada ya kibinadamu
wamekuwa wakipoteza maisha katika mazingira ambayo ukiacha yale
yatokanayo ya majanga asili yakiwamo magonjwa ya milipuko na ajali,
wengine wamepoteza maisha kwa mashambulizi yanayofanywa kwa makusudi.
Na kwa
sababu hiyo Katibu Mkuu anasema, Umoja wa Mataifa unaendelea na
jitihada zake za kuimarisha ulinzi wao ikiwa ni pamoja na
kuwajengea mazingira salama ya utendaji kazi yakiwamo mafunzo na
vifaa
Ameongeza
kuwa ushirikiano na michango kutoka nchi wanachama wa umoja wa mataifa
ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambapo siyo tu pamekuwapo na
ongezeko kubwa la mahitaji ya walinzi wa Amani na watoaji wa misaada ya
kibinadamu, lakini pia kutokana na ongezeko la mashambulizi dhidi yao
na mazingira magumu ya kazi.
No comments:
Post a Comment