Mkosi wa
majeraha umeendelea kuiandama Manchester United baada ya kushuhudia
wachezaji wake wawili wakiumia hapo jana ukiwa ni muendelezo wa majeraha
ambayo yamekuwa yakiwaandama wachezaji wa Manchester United karibu
msimu mzima .
Katika
mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la FA dhidi ya timu ya Yeovil Town
kocha Louis Van Gaal aliwashuhudia mabeki wa pembeni Rafael Da Silva na
Luke Shaw wakitoka nje huku wakiwa na majeraha yanayohofiwa kuwa ya muda
mrefu .
Beki Rafael amevunjika mfupa wa taya .
Beki wa
kulia raia wa Brazil Rafael Da Silva alipata jeraha baya ambalo
linaaminika kuwa la kuvunjika kwa mfupa wa taya baada ya kugongana
vichwa na mchezjai wa Yeovil wakati wa kuwania mpira wa juu .
Beki
mwingine wa kushoto Luke Shaw aliumia kifundo cha mguu wake baada ya
kuwa anacheza kwa maumivu kwa muda mrefu na baada ya kushindwa kuvumilia
alilazimika kutoka uwanjani.
Beki wa kushoto Luke Shaw ameumia ‘enka’.
Majeraha
haya yanafuatia majeraha ambayo yalitokea kwa Ashley Young na Antonio
Valencia walioumia kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs huku
Marouanne Fellaini akiumia kwenye mazoezi kabla ya mchezo huo .
United
bado inaendelea kuwakosa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza kutokana
na majeruhi akiwemo kiungo Mholanzi Daley Blind na beki Muargentina
Marcos Rojo.
No comments:
Post a Comment