Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam akilia huku akibembelezwa na shost yake Aunt Ezekiel.
OHOOOO!
Wakati pazia la mwaka 2014 likifungwa leo, mama la mama, Wema Sepetu
‘Madam’ ameuaga mwaka huo kwa staili ya kilio cha nguvu, mchapo hatua
kwa hatua huu hapa...
Tukio
hilo lililozua maswali mengi bila majibu, lilitokea usiku wa kuamkia
Desemba 29, mwaka huu kwenye shoo ya Madam ya kuuaga mwaka 2014 (Say
Good Bye To 2014) iliyofanyika katika Klabu 71, Tegeta-Kibaoni jijini
Dar.
Kabla
ya kukutwa na kisanga hicho kwenye shoo hiyo ambayo Madam aliiandaa
chini ya Kampuni yake ya Endless Fame, shoo mbalimbali kutoka wasanii
kibao wa Bongo Fleva kama Barnaba, Izo Business, Bob Junior na wengine
wengi zilihusika kisha baadaye Wema alipanda jukwaani na kumtambulisha
msanii wake mpya ajulikanaye kwa jina la Ally Luna.
“Ally
Luna atasimamiwa shughuli zote za kimuziki na mimi chini ya kampuni
yangu Endless Fame, na atapata huduma zote za muhimu kama inavyofanyika
kwa msanii wangu wa zamani, Mirrow,” alisikika Wema.
Mara
baada ya shoo hiyo iliyoambatana na bethidei ya mtangazaji wa Clouds
FM, Soudy Brown kumalizika, Wema alikutwa na mapaparazi nje ya ukumbi
huo akiangua kilio cha nguvu ambacho hakikujulikana moja kwa moja ni cha
nini.
No comments:
Post a Comment