Pages

December 22, 2014

SAKATA LA ESCROW LAMNG'OA PROFESA ANNA TIBAIJUKA

Rais Jakaya Kiwete akihutubia taifa hii leo katika ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam kupitia wazee wa jiji hilo. 

Pamoja na mambo mbalimbali Rais Kikwete amezungumzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchini kote na kuunga mkono maamuzi ya Waziri TAMISEMI, Hawa Ghasia juu ya maamuzi ya kuwatimua kazi, kusimamisha, kuwashusha vyema na kuwapa maonyo ya madaraja mbalimbali watendaji wote waliohusika na kuharibika kwa uchaguzi huo katika maeneo yao.

Rais Kikwete hivi amezungumzia sakata la ESCROW ambapo kwa mambo kadhaa ambayo yalikuwa yakisubiri uamuzi wake ikiwa ni pamoja na kuwaondoa mawaziri tajwa.

Rais Kikwete amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali  tayari amejiuzulu, Bodi ya Tanesco imeshamaliza muda wake na tayari ameshateua Mwenyekiti Mpya wa Bodi huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akisema amesha zungumza nae na amemuomba atupishe tuteue mwingine.

Profesa Tibaijuka anatuhumiwa kupokea kiasi cha sh 1.6 bilioni kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa VIP Engeneering,James Rugemalila kwaajili ya kusaidia shule binafsi za Prof Tibaijuka na fedha kuingizwa kwenye akaunti binafsi badala ya shule. 

Upande wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameomba amuweke kiporo yeye na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi dhidi yao.  
 

 
Wazee wa Dar es Salaam wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete katika moja ya mikutano yake na wazee jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...