Pages

December 19, 2014

MH.DANIEL FRED KIDEGA AAPISHWA KUWA SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI(EALA)

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(Eala)Daniel Kidega

Spika mpya akila kiapo bungeni leo

Spika akiongozwa na askari wa Bunge kuingia bungeni.
Bunge la Afrika Mashariki leo limefanya uchaguzi wa kumpata Spika wa Bunge hilo lenye makao yake jijini Arusha,Tanzania na kuzima mivutano iliyotawala kwa muda mrefu.

Aliyechaguliwa bila kupingwa ni Daniel Kidega kutoka nchini Uganda kuchukua nafasi ya Mh Magreth Zziwa aliyeondolewa kwenye kiti hicho siku ya jumatano wiki hii baada ya wabunge wenzake kumtuhumu kushindwa kuongoza chombo hicho muhimu.

Awali taarifa za kuaminika zilizoufikia   rweyemamuinfo.blogspot.com  zilisema majina manne kutoka wabunge wa Uganda waliochukua fomu walikua ni Daniel Kidega,Susane Nakahuki,Chris Opoka Okumu na Mike Sebaru.

Hata hivyo baadhi yao hawakurudisha fomu ya kuwania kunyanganyiro hicho huku mh Chris akiondoa jina lake na kumwachia Dan Kidega kupita bila upinzani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...