'Kreni' ilitumbukia ndani ya nyumba wakati ikimbeba mwanamume aliyekuwa anamposa mpenzi wake
Mwanamume
mmoja raia wa udachi amejikuta akikimbilia usalama wake baada ya
jaribio la kutaka kumposa mpenzi wake kwa mbwembwe kwenda mrama.
Mtu
huyo ambaye hakutajwa kwa jina anayeishi mjini Ijsselstein alikodisha
'kreni' au Crane na kuipanda akipanga kwamba kreni hilo imtoe chini na
kumpandisha hadi dirishani mwa mpenzi wake ambapo angemchezea wimbo na
kisha kumposa.
Badala yake yaliyomkuta hakuyatarajia kabisa.Kreni
hiyo ilianguka chini na kupita dirishani kwa mpenzi wake huku ikiangukia
nyumba za majirani.
Mwanamume huyo alilazimika kukimbilia
usalama wake na hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo lililowaacha
wengi wakiangua kicheko.
Kwa mujibu wa jarida la Algemeen
Dagblad, mpenzi wake mwanamume huyo alimkubali na kusema yuko radhi
kuolewa naye licha ya tukio hilo.
Baada ya kuongea na polisi, wawili hao walisafiri kwenda mjini Paris Ufaransa kusherehekea.
Kreni
hio ilianguka tena kwa mara ya pili ilipokuwa inainuliwa na hata
kuharibu zaidi nyumba za majirani. Meya wa mji huo, amezomewa na wengi
baada ya eneo hilo kusemekana kutokuwa salama.
BBC
No comments:
Post a Comment