Ofisa
wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker
Kilewa (kulia) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa
operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa
kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya
mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send”
inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi
wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva
kiwango cha pombe mwilini. Akisikiliza kwa makini ni Meneja Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto).
Ofisa
wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker
Kilewa (kushoto) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa
operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa
kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya
mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send”
inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi
wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano
wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia).
Dereva
wa basi liendalo Morogoro, John Peter, akisoma kauli mbiu ya usalama
barabarani ya mwaka 2014 katika fulana kabla ya kukabidhiwa fulana hiyo
na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia)
pamoja na stika yenye ujumbe unaohamasisha madereva kutokutumia simu zao
za mkononi wakati wanaendesha magari ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa
kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayoendeshwa na
kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika zoezi
lililofanyika leo katika mikoa ya Pwani na Morogoro. Wakishuhudia ni
Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Abigail Ambweni (wa pili toka
kulia) na Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani,
Inspekta Notker Kilewa (wa tatu toka kulia).
Mkuu
wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani
Makao Makuu, Abel Swai akisisitiza jambo kwa abiria wa basi liendalo
Iringa wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani
Morogoro leo kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania,
ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait
to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za
mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima
madereva kiwango cha pombe mwilini,Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom
Tanzania.
Ofisa
wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, PC Twaima Othman
(kushoto) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda
mikoani, Abdallah Omari (wa tatu toka kushoto) kwa kutumia kifaa maalum
wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Pwani leo
ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya
“Wait to Send” ya Vodacom Tanzania inayohamasisha madereva wa vyombo vya
moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo
hivyo. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail
Ambweni (wa pili toka kushoto).
Kampeni
ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za
usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya
Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe,leo imeendelea katika Mkoa wa Pwani na
Morogoro.
Madereva
wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia
ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms)
wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Vilevile
polisi wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani ambako ni barabara
kuu inayotumiwa na magari mengi yaingiayo na yatokayo jijini Dar es
salaam walitoa elimu kwa abiria jinsi ya kutoa taarifa waonapo vitendo
vya madereva wanaondesha magari kwa uzembe na kuhatarisha maisha yao
ambapo walipatiwa namba maalumu za simu za kutoa taarifa za matukio
hayo.
Mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani cha Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro
Boniface Mbao amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya
ajali “Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa pwani ni wengi hususani
madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo
tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa
kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema
madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali
zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi hiki
cha msimu wa sikukuu ya mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya Vodacom
kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili
ambalo limekuwa sugu .
Kwa
upande wake,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani Herieth
Koka, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali kuunga mkono
jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la
ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunatoa
rai kwa madereva wote kuzingatia kauli mbiu ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama
barabarani isemayo”Maamuzi yako barabarani ni hatma yetu-Fikiri
kwanza".
Aliongeza
kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za
kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni
ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia
sheria za usalama barabarani.
Alisema
kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa
madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es
Salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu
mbalimbali nchini.
Katika
kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa
usalama barabarani na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabani
walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha
vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha
kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya
moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi
lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendeshwa vyombo vya moto
walichukuliwa hatua kali za kisheria.
Baadhi
ya abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Pwani wamesema ni ya muhimu
itasaidia kupunguza ajali nchini.”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea
hapa nchini zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi
zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi kikubwa”.Alisema Bi Khalfan
mkazi wa Morogoro aliyekuwa safarini akitokea Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment