Pages

November 18, 2014

SERIKALI KUDHIBITI UTOROSHAJI WA MADINI AINA YA TANZANITE NCHINI

Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Ngosi Mwihava(katikati)akikata utepe kufungua Maonesho ya Tatu ya Madini ya Vito ya kimataifa mkoani Arusha leo.

Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Paul Massanja(kushoto)akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Vito jijini Arusha.

Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara kutoka nchini DRC.

Meneja Uhusiano wa Wizara ya Nishati na Madini,Badra Masoud(kushoto) akizungumza na mmoja wa wadau wa sekta ya madini nchini,Sailesh Pandit katikati ni Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Paulo Massanja.

Mwandishi wetu,Arusha
Serikali imekua ikipoteza mapato mengi kutokana na utoroshwaji wa madini aina ya Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania pekee.

Kamishna wa Madini nchini,Eng Paul Massanja amesema leo wakati wa maonesho ya madini ya Vito yanayofanyika jijini hapa ambayo yanahudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali.

Amesema kwa takwimu za mwaka 2013,Tanzania ilipata dola za marekani 38 milioni wakati nchi ya Kenya ilijipatia kiasi cha dola 100 milioni na India ilijikusanyia kitita cha dola 300 milioni.

"Wote mnafahamu haya madini yanapatikana Tanzania pekee huu ni ushahidi kuwa kumekuwa na utoroshwaji wa madini haya kwa kiwango kikubwa jambo linalotunyima mapato ya kutosha"anasema Eng Massanja


Hata hivyo amesema wataendelea kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini nje ya nchi ambayo hayajaripiwa kodi sitahili huku kukiwa na mipango ya kujenga jengo kubwa ambalo litatumika kufanyia biashara ya madini.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...