HELKOPTA ya wizaya ya Maliasili na Utalii iliyo tolewa msaada
kutoka kwa Taasisi ya Howard G.
Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw.
Warren
Buffet na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14,
2014 jijini Dar es Salaam imepata ajali na kuua watu wanne hii leo.
Helkopta aina ya Robertson R44 hiyo
ambayo baade ilikabidhiwa kwa Mamlaka ya Hifadhi za Wanyamapori
Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya
kupata hitlafu katika injili yake.
Mashuhuda
walioshuhudia ajali hiyo eneo la Kipunguni B- Ukonga Moshi Bar Ilala
Dar es Salaam waliambia Father Kidevu Blog kuwa awali waliona helkota
hiyo ikiyumba na kutoa mngurumo usio wa kawaida na baade kuzima kisha
kusikika kuwashwa bila mafaniko na baade kuanguka.
"Tulisikia
mlio wa Helkopta usio wa kawaida, na baadae ulizima na kusikika tena
kuwashwa ikagoma lakini tukasikia tu kishindo kikubwa cha Helkopta hiyo
kuanguka," alisema shuhuda huyo.
Kamanda
wa Polisi Viwanja vya Ndege, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Seleman aliambia Father Kidevu Blog kuwa walio kufa ni Marubani wa tatu
kati yao wawili ni marubani wa polisi na Afisa mmoja wa Polisi.
ACP
Selemani aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Mrakibu wa Polisi Capt.
Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa
Simba, Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Kampanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaa, Kamishna Suleiman Kova wakiwa eneo la ajali.
Picha ndogo ni Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala enzi za uhai wake.
Watu wa usa;lama wakiwa eneo la tukio.
Helkopta hiyo ilivyo haribika.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Helkopta hiyo ilivyo haribika.
No comments:
Post a Comment