Wafanyabiashara
wa Namanga na Wilaya ya Longido wameiomba Serikali iwajengee Soko kubwa
Namanga ili waepukane na usumbufu wanaoupata wanapokwenda Kenya kuuza
mifugo, mazao na bidhaa nyingine.
Wafanyabiashara
hao walitoa ombi lao jana Septemba 19 wakati wa mkutano na Maofisa wa
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaotembelea mipaka
mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Mtangamano wa Afrika Mashariki.
Baadhi
ya manyanyaso wanayopata wanadai ni kuombwa kitu kidogo, kupewa malipo
kidogo ya bidhaa zao kuliko bei ya soko na kusumbuliwa kuhusu ubora wa
bidhaa wakati bidhaa zao zimetimiza viwango vyote.
Uongozi wa Wilaya ya Longido umetenga eneo la heka 120 kwa ajili ya soko ili wafugaji na wakulimna wauzie bidhaa zao hapo.
Hiyo
pia itasaidia Wanunuzi kutoka Kenya waje kununua sokoni hapo na hivyo
wakulima na wafanyabishara wa Tanzania kupata bei nzuri na kuepuka
usumbufu wanaoupata sasa.
Wafanyabishara
hao pia wamesema ujenzi wa soko utasaidia kuzuia Wakenya kwenda
mashambani na kununua mazao moja kwa moja kwa wakulima.
Akizungumza
na wafanyabiashara hao Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Ufuatiliaji na
Tathmini kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Graceana
Shirima alisema Serikali itashugulikia haraka malalamiko yao ikiwa
pamoja kuharakisha ujenzi wa masoko mipakani.
Shirima,
ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Joyce Mapunjo, alishauri uongozi wa
Wilaya ya Longido kuanza na utaratibu wa gulio wakati wakiendelea na
mikakati ya ujenzi wa soko.
Mweka
Hazina wa Wilaya Issai Mbiru alisema tayari Wilaya imepata fedha
Shilingi bilioni 2.3 kutoka kwa wafandhili na ujenzi wa soko hilo
utaanza muda si mrefu.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara Bi. Graceana
Shirima (kulia) akimkabidhi machapisho mbalimbali Katibu Tawala wa
Wilaya ya Longido Bw. Dunford Peter wakati wa ziara ya kuonana na
wafanyabiashara wa Namanga tar. 19-9-2014
Malori
yakisubiri kukamilisha taratibu za kuvuka Mpaka wa Namanga kuingia
Tanzania kwa kutumia utaratibu wa zamani. Ujenzi wa OSBP utarahisisha
Malori na wasafiri kupita.
Jengo
la Utoaji wa Huduma za Pamoja Mpakani (OSBP) Namanga (upande wa nyuma)
likiwa katika hatua za mwisho kukamilika. OSBP inatarajiwa kupunguza
urasimu wa kuvuka mipakani.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini (katikati) akisikiliza
malalamiko ya wafanyabiashara wa Namanga tar. 19-9-2014. kushoto ni
Mchumi Othman Chanzi na kulia ni Katibu Tawala, Longido Dunford Peter.
Baadhi
ya Wafanyabiashara wa Namanga na Longido wakiwa katika mkutano wa
pamoja na Wizara kuhusu kufuatilia kero wanazopata mipakani. Mkutano huo
ulifanyika tarehe 19-9-2014. Wengine ni wawakilishi wa SIDO, TAHA na
TCCIA Mkoa wa Arusha.
No comments:
Post a Comment