Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Margareth Sitta akifungua semina ya
Wanawake iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi,
utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13
Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana
akiwahutubia baadhi ya wanawake na wanaume waliohudhuria semina maalum
iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa
migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba,
2014 mjini Dodoma.
Mwakilishi
wa Shirika la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
akichangia mada wakati wa semina ya wanawake iliyofanyika leo 13
Septemba, 2014 ambayo ikihusu iliyohusu kuwawezesha wanawake katika
masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi
iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia
uwasilishwaji wa mada toka kwa viongozi wakati wa semina hiyo. (Picha
zote na Edwin Mjawahuzi)
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
Katika
juhudi za kuleta usawa wa kijinsia na kuinua hadhi ya wanawake,
Serikali imefanya jitihada kubwa katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na
kijamii licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali katika jitihada hizo
Hayo
yamesemwa 13 Septemba, 2014 na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana wakati wa semina iliyohusu masuala ya
kuwapa nyenzo ama uwezo wananawake waweze kushiriki vizuri katika
maeneo mbalimbali yanayowakilisha wanawake huku wakiungwa mkono na
wanaume.
Mhe.
Chana amesema kuwa baadhi ya watu nchini wamekuwa na dhana tofauti huku
wakiona wakipotezewa muda pindi mambo yoyote yanayowahusu wanawake
yanapozungumzwa wakisahau kuwa ili taifa liweze kufika mahali pazuri na
kuwa na maisha bora kwa kila Mtanzania hakunabudi kulitazama kundi hilo
la wanawake ambalo ni muhimu.
Mhe.
Chana ameeleza kuwa asilimia 51% ya Watanzania ni wanawake ambao
wanachangia nguvu kazi kwa upande wa kilimo kwa asilimia 45 ya pato la
Taifa, pia asilimia 25 wako katika ajira iliyo rasmi lakini wengi wako
katika sekta isiyo rasmi.
“Asilimia
34% pia ya wanavyuo kutokana na takwimu inaonyesha kwamba ni wanawake,
kwahiyo ajenda ya wanawake haikwepeki”, alisema Mhe. Chana.
Akizungumzia
kuhusiana na masuala ya mchakato wa kusaka Katiba Mpya, Mhe. Chana
amesema kuwa katika majadiliano yanayohusu Katiba, ajenda ya wanawake
pia haikwepeki.
Mhe.
Chana aliongeza kuwa endapo wanawake nchini watawezeshwa basi taifa zima
litakuwa limewezeshwa kwani watu wengi waliopata mafanikio ni kutokana
na wanawake kutoa malezi bora katika kulea watoto pindi wanapozaliwa
hadi kupata elimu.
Aidha,
Mhe. Chana amesisitiza juu ya wanawake kushirikishwa katika vyombo vya
maamuzi ili kuongeza hali ya uchumi kwa wanawake, hali ya kijamii ya
wanawake na ya kisiasa kwa wanawake hao.
“Lazima
tuwepo kwenye vyombo vya maamuzi kwani ndiko tunapopata haki zetu kwani
huko pia ndiko tunapoweka bajeti ya serikali kuu, bajeti ya serikali za
mitaa, kwahiyo tunaanza na vyombo vya maamuzi”, alisisitiza Mhe. Chana.
Naye
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya amesema kuwa
Tanzania ina wanawake wenye sifa, na uwezo na maarifa kwenye maeneo yote
kuanzia, udaktari, uhasibu, Wahandisi yakiwemo na maeneo mengine.
Ameongeza
kuwa, ajenda ya kufikia hamsini kwa hamsini kwa wanawake haina mjadala,
hivyo wanawake wana haki ya kuhusishwa katika masuala ya ungozi kama
ilivyo kwa wanaume.
“Mwanamke
kwenye uongozi ni lazima aweze kuliko mwanaume, anatakiwa ajiwekee
mikakati yake mwenyewe ya kujihudumia (selfcare) ili kuwa na muda wetu
wenyewe”, alisema Bi. Mallya.
Bi.
Mallya aliongeza kuwa wanawake wanapaswa kutambua kuwa ajenda inayohusu
mapambano ni ajenda ya muda mrefu ndani ya maeneo yao ya uongozi.
Bi
Mally alisisitiza kuwa, wanawake wajitahidi kuwa wanasiasa kwenye vyama
vya siasa, wawe wabunge pia wawe viongozi kwenye taasisi za umma na
binafsi ili kufanikisha suala lao la hamsini kwa hamsini.
No comments:
Post a Comment