Pages

September 12, 2014

MWANARIADHA MLEMAVU ALIYEMPIGA RISASI MPENZI WAKE AFRIKA YA KUSINI.

 
Jaji Thokozile Masipa kushoto anayehukumu kesi ya mwanariadha mlemavu Oscar Pistorious.

Akiwa mahakamani, ambako amekuwa akisikiliza kesi ya mwanariadha mlemavu Oscar Pistorious tangu marchi, jaji Thokozile Masipa amekuwa akionekana kama mtu ambaye fikra zake ziko mbali, mtulivu na mtu anayetazama mambo kwa undani.


Akiwa amevalia miwani, jaji huyu hajizuii kuzungumza mengi na mara nyingi hutabasamu tu.

Tangu mwanzo wa kesi hii, wakosoaji wake ambao wengi ni wanaume, wamekuwa wakinadi kuwa kujitenga kwake ni ishara kuwa hana ufahamu wa kutosha au kutishwa na vyombo vya ahabari ambavyo vimekuwa vikitangaza vikao vya kesi hiyo moja kwa moja.

Wakili mmoja nchini afrika kusini Jeremy Gauntlett alinukuliwa akisema kuwa jaji Masipa ana wasi wasi mwingi kutokana na kuwepo kwa waandishi wa habari mahakamani.

Huku kesi hii ikimalizika, utulivu wa jaji Masipa, ukilinganisha na vilio na sarakasi zilizokuwa mahakamani kutoka kwa watu waliokuwa wakilia mara kwa mara wengi wao wanaume wazungu, jaji Masipa amepata sifa nyingi na heshima ya hali ya juu.

Alijiepusha kuingilia kati mawakili walipokuwa wakiwasilisha ushahidi au wakati walipokuwa wakiwahoji mashahidi na mshtakiwa, lakini kila alipoingilia wengi walifurahiswa na umaakini na usawa ambao alikuwa akiuonyesha kwa pande zote.

Jaji huyo ni mmoja wa watu waliopata wakati mgumu sana wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi na miongoni mwa wale waliotambua kuwa maisha sio kazi unayofanya au malengo maishani bali ni kufanya taifa lako kuwa nzuri alisema jaji mmoja wa mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini Albie sachs.

Thokozile Matilda Masipa, mwenye umri wa mia 66, ametoka mbali.

'Ametoka mbali' Oscar Pistorius akisindikizwa mahakamani

Alizaliwa katika kitongoji kimoja nje ya mji mkuu wa Johannesburg na wakati mmoja aliajiriwa kama karani na mpishi wa chai.

Kwa wakati mmoja nusura aachane na masomo yake kwa kuwa alidhani kuwa hatafanikiwa kwa vyovyote vile licha ya masomo aliyonayo.

Lakini mamake aliendelea kuumpa motisha ya kuendelea na masomo yake. Alikwenda chuo kikuu na baada ya kumaliza aliajiriwa kama mwandishi wa habari kabla ya kufungwa jela wakati ya vita vya ukombozi.

Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, jaji masipa alirejea tena chuo kikuu ambako alisomea uanasheria, wakati huo afrika kusini ilikuwa imeanza kuzingatia utawala wa demokrasia.

Aliteuliwa jaji mwaka wa tisini na nane na kuwa mwafrika wa pili wa kike kuwahi kuteuliwa jaji nchini Afrika Kusini.

Lakini tangu kesi ya Pistorious kuanza, wengi wamekuwa wakichunguza hukumu ambazo amezitoa kati kesi zilizopita.

Mwaka wa 2009, alimhukumu afisaa mmoja wa polisi kifungo cha maisha gerezani baada ya kumpata na hatia ya kumuua mke wake wa zamani. Alisema hakuna aliye juu ya sheria na kuwa afisa huyo anastahili kwenda jela kwa kushindwa kutii sheria.

Mwaka uliopita alimhukumu mwanamme mmoja miaka 252 gerezani baada ya kumpata na hatia ya kuwabaka wanawake watatu katika makaazi yao.

Akiwa mahakama hamna anayeweza kujua fikra za jaji masipa na oscar pistorious haweza kufahamu hata yake kamili licha ya jaji huyo kutompata na hatia ya kumuua mpenzi makusudi, Itabidi pistorious kusubiri hadi jaji huyo atakapomaliza kusoma hukumu yake.bbc

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...