Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe,kutangaza mgomo na Maandamano nchi
nzima kwa ajili ya kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe mara moja kwa
madai Bunge hilo limeshindwa kutengeneza katiba ya Nchi, badala yake
linatunga Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM, Naye
Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameibuka na Kumvaa
Mwenyekiti huyo wa Chadema Freeman Mbowe na kusema Jeshi hilo
halitakubali kuona amani ya nchi inavurugwa.
Kwani Maandamano hayo pamoja na migomo ni kinyume cha sheria
na kanuni zinazosimamia Jamii kutii sheria na utaratibu wake.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam Kamishina wa polisi
Oparesheni na Mafunzo Paul Chagonja -CP kwa Niaba ya Mkuu wa jeshi la
polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari
kuzungumzia kauli aliyoitoa Kiongozi huyo wa Chadema,ambapo Chagonja
alisema Jeshi hilo halitakubali kushuhudia Migomo na Maandamo yenye
kulenga kuvuruga Amani
“Jeshi la polisi tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli
aliyoitoa Freeman Mbowe kwamba yeye pamoja na wafuasi wake wa chama
chake wanajipanga kufanya maandamano na migomo isiyokomo nchi nzima bila
kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi ili kushinikiza Bunge la
katiba kuhailishwa ,sisi jeshi la polisi tunaonya vikali kauli hiyo
ambayo ni kinyume cha taratibu za nchi na hatutakubali”alisema
CP-Chagonja
Chagonja alizidi kusema ieleweke wazi kwamba siasa zina mipaka
na zinapovuka mipaka hiyo na kuanza kwenda kinyume cha sheria,kanuni na
taratibu za nchi hiyo inageuka kuwa jinai na wala siyo siasa tena.
Aidha Chagonja alisema Jeshi hilo la polisi aliweza kumvumilia mtu
yeyote atakayetumia mwavuri wa siasa kutaka kuvuruga Amani na utulivu
uliopo hapa nchini na Jeshi halitasita kumchukulia hatua kali kama
mhalifu Mwengine yeyote.
Katika hatua nyingine Jeshi la polis limewataka wananchi wote
kufuata sheria na taratibu za nchi na kuepuka kauli zenye kulenga
kuvuruga Amani ya nchi.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi nchini limekuja siku moja baada ya
Mwenyekiti waChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe
kutangaza kuwepo kwa maandamano bila kikomo nchi nzima kushinikiza
kusitishwa kwa Bunge la Katiba aliloliita la kifisadi linaloendelea
mjini Dodoma.
Pia, Chama chake kimeazimia kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya
urais ifikapo mwakani, lengo likiwa kuung’oa utawala wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), uliowafanya watanzania kuwa maskini wa kutupwa.
Akihutubia mkutano mkuu wa uchaguzi, Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Taifa,
Freeman Mbowe, alisema umefika wakati sasa wa kuacha kukaa na kuzungumza
na kwani kinachoendelea Dodoma ni wizi na ukatili wa hali ya juu kwa
wananchi wanyonge ambao ndio walipa kodi.
“Samahani maneno yangu ni makali na wala hapa sifanyi
uchochezi…kinachoendelea Dodoma ni ufisadi na wizi, tumekaa Kinana,
tumekaa na Mangula, tumekaa na Rais Kikwete tumekubaliana bunge
lisitishwe lakini wanamwacha Sita afanye anachotaka kama utafikiri ndiye
Rais…
“Anachakachua rasimu, anabadili kanuni, anavunja sheria anakusanya
maoni utafikiri yeye ni Warioba…hiki hakivumiliki, naomba mkutano huu
utoke na tamko,” alisema Mbowe na kushangiliwa na wajumbe wakiafiki.
No comments:
Post a Comment