Pages

September 9, 2014

JAJI MSTAAFU AGUSTINO RAMADHANI ACHAGULIWA KUWA RAIS WA MAHAKAMA YAHAKI ZA BINADAMU

JAJI  Mstaafu wa Tanzania,Agustino Ramadhani amechaguliwa kuwa rais wa
 Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika(AfCHPR) , kwa kipindi cha
miaka miwili hadi  mwaka 2016.

Pia katika  jopo la majaji hao   Elsie Thomposon kutoka Nijeria  naye
ameibuka kidedea kwenye uchaguzi huo uliofanyika juzi katika   viwanja vya
mahakama hiyo na kushika nafasi ya kuwa makamu wa Rais wa mahakama
hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uchaguzi huo kuisha,
Jaji Mstaafu Ramadhani alishukuru kwa majaji wenzake kumchagua
kuiongoza mahakama hiyo kwa kipindi hicho.

Aidha alisema kuwa katika  nafasi aliyoipata ni sifa kubwa kwa nchi ya Tanzania na nchi
za Afrika kwani  kwa Tanzania nafasi hiyo ni  changamoto ya
kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kuheshimiwa na kila mtu.

“Nawashukuru wenzangu kwakuniichagua na pia hii ni sifa kwa nchi yangu
na  wenzetu wakiona tunafaa kuongoza  tunaweza  tena mara baada ya
kumaliza  nafasi zetu mwaka 2016 , hivyo hii ni heshima kwa Taifa
letu”.

Jaji Ramadhani amepata nafasi hiyo mara baada ya  aliyekuwa Rais wa
mahakama hiyo,  Jaji Sophia  na  Akkufo  kumaliza muda wake.

Awali kulitanguliwa na kuwaapisha majaji wengine wapya watatu ambao ni
 Jaji Rafaa Achour kutoka Jaji Solomy Basa ,  pamoja na Jaji  Angelo
Mahesa  ambao wameapishwa jana kuziba nafasi zilizoachwa wazi na
majaji wengine watatu waliomaliza muda wao akiwemo Akuffo .

Halfya ya kuapishwa kwa  majaji hao pia ilihudhuriwa na viongozi wa
dini kutoka mahehebu mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali.

Mara baada ya kuapishwa kwa majaji hao na uchaguzi  kumalizika  Rais
wa mahakama hiyo, Jaji mstaafu   Ramadhani alisema kuwa kazi ya
mahakama hiyo ni kusimamia haki za binadamu pamoja na kuhakikisha
inatoa maamuzi katika kesi mbalimbali zilizofikishwa mahakamani hapo .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...