Pages

September 2, 2014

CHAMA CHA MAPINDUZI UINGEREZA CHAPATA MWENYEKITI MPYA


KAPINGA KANGOMA MWENYEKITI MPYA CCM UK - AIBUKA NA USHINDI WA KISHINDO  WA ASILIMIA 94.6% YA KURA ZOTE HALALI.

Aanza kwa kuunda timu itakayounda upya Jumuiya ya Watanzania UK na kuhusisha wadau wote;Azungumzia suala la uraia pacha na Rais Ajaye katika uchaguzi 2015;Kuunda Saccoss ya watanzania UK na Jumuiya ya Wanawake.Na Abraham Sangiwa Itikadi Siasa na Uenezi - CCM – UNITED KINGDOM.

 Mwenyekiti Mpya wa CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma akitoa nasaha na shukrani zake.
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM UK Ndugu Maina Owino akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti Mpya CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma.
 Wajumbe, wanachama wa CCM UK na watanzania waishio uingereza wakimsikiliza Kwa makini Mwenyekiti Mpya wa CCM Ndugu Kapinga Kangoma (hayupo pichani).
 Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Maina Owino akipiga kura yake katika Uchaguzi wa Mwenyekiti Mpya wa CCM UK.
 Kaimu Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela(mwenye koti jeupe) akichukua taarifa ya yanayojili katika mkutano huo pembeni yake ni Ndugu John Lyimo Katibu wa Uchumi na Fedha CCM UK.
  Katibu Itikadi Siasa na Uenezi CCM UK Ndugu Abraham Sangiwa akitekeleza haki yake ya kikatiba kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti Mpya CCM UK.
 Meza kuu ikimkaribisha Mwenyekiti mpya wa CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma kuchukua Nafasi yake kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti CCM UK Ndugu Sukwa Said Sukwa, Mwenyekiti mstaafu Maina Owino na Abraham Sangiwa – Itikadi na Uenezi CCM UK.
 Katibu wa CCM Shina la Birmingham Bi. Lilian Barongo ambaye pia anakuwa Katibu mteule wa Jumuiya ya Watanzania UK Akibadilishana mawazo na Kaimu Katibu wa CCM UK  Ndugu Leybab Mdegela kabla ya kuingia katika ukumbi wa mkutano
 Wanachama, wajumbe na watanzania waliohudhuria mkutano wakipata maankuli ya ukweli.
 Café 12 misosi na vinywaji palikuwa hapatoshi.
Baadhi ya wanachama na watanzania walipatiwa uhakiki kabla ya kuingia ukumbini.


==============
Mkutano mkuu wa wanachama wote CCM UK ambao uliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM UK umefanyika katika jiji la Reading siku ya Jumamosi tarehe 30/08/2014 ambapo wagombea watatu walipitishwa na vikao vya awali kugombea nafasi hiyo ni Ndugu Said Surur, Peter Gabagambi na Kapinga Kangoma na kujaa shamrashamra na nderemo na  kuhudhuriwa na wanachama wa CCM UK NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA pia viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM aliyeng”atuka Ndg  Maina Ang'iela Owino, Makamu Mwenyekiti  Ndugu Said Sukwa, Kaimu Katibu Ndugu Leybab Mdegela,  Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa, Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi na Fedha Ndugu Mohamed Upete, Viongozi wa mashina, wajumbe na wanaCCM toka mashina ya CCM UK.

Mkutano huo ulianza kwa  Katibu mwenezi ndugu Abraham Sangiwa kuwashukuru Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi hapa UK ili kuleta chachu ya mabadiliko ndani na nje ya chama kwa manufaa ya watanzania wote kwa ujumla.

Ndg Sangiwa aliwakumbusha kuwa kujiunga na CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.

Akimkaribisha Mwenyekiti mstaafu Ndugu Maina A Owino, Kaimu Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela aliwashukuru wanachama wote kwa kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha malengo ya mkutano huo na zoezi la kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM UK na kuwafahamisha wanachama wagombea wawili Ndugu Said Surur na Peter Gabagambi waliopitishwa na vikao vya awali wamejitoa katika kinyanganyiro hicho hivyo mgombea pekee aliyebaki katika nafasi hiyo ni Ndugu Kapinga Kangoma, pia ripoti ya Tawi iliwakilishwa na itasambazwa na viongozi wa mashina kwa wanachama wote.

Katika hotuba yake Mwenyekiti mstaafu Ndugu Maina A Owino aliwashukuru wana ccm na watanzania wote kwa ujumla kwa ushirikiano waliompa katika awamu yake ya kwanza ya uongozi tangu kuanzishwa kwa tawi hapa UK ambapo awamu yake imefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wana CCM na watanzania kwa ujumla katika miji mbalimbali hapa UK ; Aidha alisema baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko endelevu, kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na kwamba CCM na serikali yake inaendelea kujiimarisha kuyakabili kwa mikakati na mipango endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina aliwakumbusha Wana CCM UK Kuwa mchango wao unahitajika na ni wamuhimu katika kuleta mabadiliko yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali muhimu za kimaendeleo na kichumi kuanzia na watanzania wanaoishi hapa UK na nyumbani.


Katika hotuba yake ya ushindi Mwenyekiti Mpya wa CCM UK ndugu Kapinga Kangoma aliwashukuru wana CCM UK kwa Imani waliyoionyesha kwake na kumpa kura za ushindi na kusema “hakika kwangu na familia yangu ni heshima kubwa. “
Sasa tuna kila sababu ya kuanza awamu ya pili ya Uongozi wa CCM UK Kuunganisha maisha ya watanzania hapa UK na diaspora kwa ujumla na kutengeneza platform itakayoleta uongozi mahiri kuelekea hiyo awamu mpya, hivyo napenda kuwajulisha kwamba awamu hiyo imeanza leo kwa kunichagua mimi kuwa mwenyekiti wenu.
Ninaanza kazi yangu kwa kuunda upya Jumuiya ya watanzania hapa UK hivyo CCM UK itaweka uzito wote unaostahili kuhakikisha kuwa tunaunda jumuiya itakayotokana na Watanzania wenyewe na sio kushirikiana na ubalozi.. hatutaki tena kukaa na ubalozi eti kutengeneza jumuiya ya Tanzania hapa UK, uzoefu unaonyesha kuwa tukishakuwa na ubia na ubalozi malengo ya jumuiya yanakuwa sio endelevu..hasa kama anapatikana balozi ambaye hana interest na jumuiya za Kitaanzania; basi inakuwa rahisi sana kuibomoa. Hivyo leo naanza kazi kwa kuunda jumuiya ya watanzania hapa UK, ambayo itafanya kazi ya kuunganisha mikakati na taasisi zingine zenye malengo tofauti na CCM (hapa UK) ili mradi mwisho wa siku waje na jumuiya ambayo haina harufu ya serikali japo watafanya kazi na ubalozi kama wadau pale inakapobidi na terms and conditions will-apply. Hivyo namteua bwana Abdulaziz Jaad kuanza mchakato huo yeye ni msomi mzuri na ana uzoefu wa hapa na kule nyumbani kwani sehemu zote mbili ameshafanya kazi kwenye taasisi mbalimbali nitamsaidia kwenye kila hatua ili afanikiwe na jumuiya ipatikane haraka. Naomba nimtambulishe kwenu ili mtakapomuona analeta mapendekezo kwenye miji yenu msimwangushe ili tuanze rasmi kutumikia kizazi chetu na kijacho; kwa kuanzia atasaidiwa na Hussein Chang’a toka Reading na katibu wa kamati hiyo atakuwa Mwanasheria Lilian Barongo toka Birmingham; wote hao ni wasomi wazuri sana nina hakika watakuja na SCIENTIFIC APPROACH kuhusu suala hilo.

Suala la pili ni kuifanya diaspora kuwa soko au kutumia fursa za sanaa kwa vijana wetu wa nyumbani na wa hapa ili kuendeleza vipaji walivyonavyo kwa kuunganisha soko la UK la music na sanaa zingine na lile la nyumbani. Mfano ni wenzetu wa nchi kama Nigeria na hata Ghana ambapo diaspora zao zimeshiriki katika kutambulisha vipaji vya nchi zao katika masoko ya dunia. Hivyo diaspora ya Tanzania lazima ifanye kazi za kuunganisha masoko ya nchi zetu kwa kuanza kufungua njia za bidhaa mbalimbali ikiwemo sanaa. Nitaunda timu ya vijana wa ccmUK na wengineo ili waanze kuandaa strategy ya mpango huo na timu nyingine ambayo itaanza kujenga mfumo wa kuunganisha mtandao wa masoko ya bidhaa mbalmbali kwa kutumia mtandao wetu hapa UK.

CCM na rais ajaye..
Ndugu wana-CCM-UK na watanzania wenzangu kama mnavyojua kwamba nchi yetu mwaka ujao itaingia kwenye kinyang’anyiro cha kumpata rais mpya baada ya mchapa kazi Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kikatiba..na kwa vyovyote ccm ndio itakayoleta rais mpya..kwani vyama vingine bado vina safari ndefu mpaka kuja kuongoza TZ. Na tukumbuke kuwa rais ndiye muhimili wa mambo yote ndani ya nchi na hivyo akija rais bomu mafanikio yaliyopatikana katika nchi yetu yatapotea...niwakumbushe tu kuwa rais anayemaliza muda wake ametekeleza vizuri sana majukumu yake yaliyomo kwenye ilani ya uchaguzi hivyo chama kinahitaji mtu bora zaidi ya Jakaya ili aweze kuendeleza pale atakapoishia Jakaya kikwete. Na sasa nchi ipo kwenye hatua za mwisho za kuanza kuuza gesi na labda baadae mafuta hiyo ni changamoto kubwa sana kwa rais ajaye. Sasa kuna makundi mengi yanayojionyesha kuutaka urais wa kupitia chama chetu na wote wanasifa mbalimbali kikubwa sio wao kujinadi maana mtu akijinadi hataji mabaya yake atajisifia na kuonyesha mambo yako safi..kumbe anaficha mambo mengi na ukichukulia watanzania  wa vijijini hawana uwezo wa kuwang’amua na kuwapembua..Hivyo diaspora ya Tanzania tuna jukumu la kusaidia kupeleka  pressure kuhakikisha watu wenye dhambi na wasio na uwezo wasipate nafasi hiyo nyeti. Issue hapa sio tu ufisadi bali pia uwezo wa kuongoza nchi. Maana mtu anamsema mwenzake kuwa ni fisadi as if kipimo tumeshakiweka kwamba kama wewe sio fisadi basi hata kama ni mjinga basi unaruhusiwa kuupata urais wa Tanzania; Hiyo sio kweli;  we need a capable person with integrity. Sisi hapa UK na sehemu zingine za huku ughaibuni tunawajua sana hawa viongozi kwani wanafika sana na tumeshaongea nao mara nyingi. Authenticity zao tunazijua, How reliable they are tunawajua, lakini pia tuna access ya information kuliko wale wa vijijini..hivyo tukinyamaza hatuitendi haki jamii yetu na tunaongeza mzigo kwa watoto wetu hapo baadae waanze tena kupambana na majanga hayohayo ya viongozi wabovu kwani tukiwaacha leo bila ya kuwasema watawaweka na hata watoto wao... hivyo ninaunda idara ya siasa ambayo itaratibu matamko mbalimbali ya kichama yenye lengo la kujenga na sio kumhujumu mtu yeyote.. 

Hope hiyo itasaidia kujenga siasa bora ndani ya chama cha mapinduzi. Nitaboresha idara ya fedha ili kuhakikisha chama kinajitegemea ikiwa ni pamoja kuanzisha SACCOS itakayoanza kujenga mitaji ya biashara na hata baadae kuwa na benki yetu hapa UK maana tunaweza kuwa na skills lakini bila mitaji inabaki kuwa ndoto za alinacha. Pia nitaimarisha idara ya miradi ili iweze kusaidia kuingiza  ideas za watu mbalimbali kwenye uchumi wa chama kwa ubia na watu hao. Hivyo wanachama mnakaribishwa kuleta ideas zenu. 

Nitaboresha pia idara ya wanawake na watoto ili kupata mchango kutoka kundi letu muhimu na mnajua uki-mpromote mwanamke umemsaidia pia mtoto. Hivyo mchango wa jumuiya ya akina mama tunaihitaji sana hapa ccm UK. Sijapata mtu wa kuziba nafasi hiyo nitashauriana na wadau wenzangu kumpata mama atakayefaa kusuka jumuiya hiyo ya chama na kuieneza kwenye kila mji ambao una shina la ccm,,ndo maana sikuweza kukurupuka na jina lolote ili kuleta maana nzuri ya nafasi hiyo. Jina au team nzima ya UWT itafuata baadae.


Mwisho nimalize kwa hoja ya uraia pacha kwani hivi karibuni mheshimiwa rais wa Tanzania amekuwa na nafasi mbalimbali za kuzungumzia diaspora, kwanza kule marekani na hatimaye juzi pale Dar es salaam. Mambo muhimu aliyoongelea ni kuhusu watu wa diaspora kuto kuongelea mambo yetu kwa uzito unaostahili. Japo sikubaliani na mhesh. 

Rais kuhusu dhana ya kuwakataza wana-diaspora kuhoji mambo mbalimbali ya nyumbani kitu ambacho ni haki yetu ya msingi,,lakini naomba pia nimuunge mkono mhesh.Rais kwamba ni kweli Watanzania wa diaspora hatujahamasika vya kutosha na kushiriki kwenye uwanja wa habari muhimu za mambo yanayotuhusu bali tumekuwa wepesi wa kujadili mambo madogomadogo tu.

wengi wetu ni wepesi sana wa kutoa kauli nzito vichochoroni lakini hatufanyi hivyo hadharani. Woga huu lazima tuuache kwani hoja zisipojadiliwa na mzazi zinabaki zikimsubiri mtoto wako akue halafu aje afanye kazi hiyohiyo!!!kwanini tusimalize majadiliano sasa? Hivi sasa kwenye mitandao ya jamii kuna hoja nyingi zinajadiliwa na watu walioko nyumbani wakiituhumu diaspora na kuonyesha kuwa hatupaswi kupewa uraia pacha kwani nchi haitakuwa salama..

lakini hoja za kuhoji mantiki hiyo zinakuwa chache sana kutokea upande wa diaspora. Hivyo nichukue nafasi hii kuwahimiza tuongeze kasi ya kutumia mitandao ya kijamii kwani hoja zinazotuhusu zinaandikwa na watu wengine na hivyo wanapotosha. 

Nawashukuruni sana wote naomba nifunge kikao na turejee kwenye miji yetu salama.

IMETOLEWA NA ABRAHAM SANGIWA IDARA YA ITIKADI, SIASA NA UENEZI CCM TAWI LA UINGEREZA
01.09.2014.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...