Katika kuweka msisitizo juu ya tamko lao juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014, umoja wa Asasi Nne zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimefanya matembezi huru kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Maandamano hayo
yamewahusisha pia wanafunzi wa shule za sekondari za Jitegemee, Kinyamwezi, Ilala,
Chanika na Maji ya Chai.
Picha ya pamoja ya wanafunzi na viongozi wa asasi za kiraia walioshiriki matembezi hayo huru ili kuweka msisitizo juu ya tamko juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa
Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014
Afisa Miradi wa Forum CC, Fazal Issa aliyeshika kipasa sauti akifafanua jambo kwa wanafunzi walioshiriki matembezi hayo
Matembezi huru yakiendelea
Msimamizi
wa idara ya Habari ya YouthCAN, Dickson Daniel akizungumza na wanafunzi
walioshiriki matembezi huru ya kuunga mkono na kusisitizia tamko la
asasi za kiraia juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa
Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014
Meneja
Ushawishi wa Oxfam, Eluka Kibona akizungumza na wanafunzi walioshiriki
matembezi huru ya kuunga mkono na kusisitiza tamko la asasi za kiraia
kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi
utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014
Mratibu wa CAN Tanzania, Sixbert Mwanga akifafanua jambo wakati wa matembezi
huru ya kuunga mkono na kusisitiza tamko la asasi za kiraia kuhusu
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika
huko New York-Marekani Septemba 23, 2014
Wanafunzi wa Jitegemee katika picha ya pamoja
Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Ilala, Mwanaidi Ibrahim akiimbisha wimbo wa mazingira wakati wa matembezi huru ya kuunga mkono na kusisitiza tamko la asasi za kiraia kuhusu
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika
huko New York-Marekani Septemba 23, 2014, pembeni yake ni Afisa Miradi wa ForumCC, Fazal Issa
No comments:
Post a Comment