Watanzania
waliopata ufadhili wa masomo nchini China katika ngazi ya shahada ya
uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi wakiwa katika picha ya
pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
(katikati) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa
nne kutoka kushoto mstari wa nyuma) pamoja na watendaji wengine wa
Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kuagwa rasmi katika Makao
Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.Wengine katika picha (mstari wa
mbele) ni Kamishna Msadizi Nishati anayeshughulikia Umeme, Eng.Innocent
Luoga (wa kwanza kulia), Kamishna wa Madini, Eng.Paul Masanja (wa pili
kulia), Kaimu Mkurugenzi Utawala – Bi. Caroline Musika (wa kwanza
kushoto).
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa tano kutoka kushoto
waliosimama), akiwatambulisha wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo
nchini China (baadhi hawapo pichani) waliofika Makao Makuu ya Wizara ya
Nishati na Madini na kukabidhiwa nyaraka zitakazowawezesha kujiunga na
masomo nchini China.Wanaowatazama wanafunzi hao ni Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Utawala na Rasilimali Watu, Caroline Musika (wa kwanza kushoto,
waliokaa), Mkurugenzi Msaidizi-Rasilimali Watu, Lusius Mwenda (wa kwanza
kulia),Kaimu Kamishna Msaidizi,Maendeleo ya Nishati, Eng. Juma Mkobya
(wa pili kutoka kulia), Kamishna wa Madini, Eng. Paul Masanja (kushoto
kwa Mhe.Waziri).Wengine katika picha ni watumishi kutoka Wizara ya
Nishati na Madini na waandishi wa habari.
Bi.
Erasma Rutachura, ambaye amepata ufadhili wa masomo nchini China,ngazi
ya shahada ya uzamivu katika mafuta na gesi akipokea nyaraka
zitakazomwezesha kujiunga na masomo yake mwaka huu.Anayempa nyaraka hizo
ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili
kutoka kulia).Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na
Madini, Eliakim Maswi.
Serikali
ya China kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa ufadhili wa nafasi
kumi (10) za masomo kwa watanzania katika ngazi ya shahada ya uzamili na
uzamivu katika fani ya mafuta na gesi.
Katika
shahada ya uzamili wamechaguliwa watanzania 9 kati ya 46 walioomba
ufadhili ambapo katika shahada ya uzamivu amechaguliwa mtanzania mmoja
kati ya wanne waliowasilisha maombi.
Msaada
huu wa masomo umetolewa na Serikali ya China kwa Tanzania kufuatia
juhudi za Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa
na rasilimaliwatu ya kutosha katika kusimamia Sekta za Nishati na Madini
hasa sekta ndogo ya mafuta na gesi inayokua kwa kasi hapa nchini.
Ufadhili
huu ni wa pili kupitia Wizara ya Nishati na Madini ambapo wa kwanza
ulitolewa katika mwaka wa fedha 2013/14 kwa nafasi 10 katika ngazi ya
shahada ya uzamili kwenye fani za nishati na madini ikiwemo uhandisi
migodi, uhandisi wa nishati katika mafuta na gesi. Wanafunzi hao
wanatarajia kuingia mwaka wa pili wa masomo mwezi septemba, 2014.
Nafasi
hizi zimepatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya
habari ambapo vigezo vilivyotumika kupata ufadhili ni aina ya kozi
aliyoisoma mwombaji katika Shahada ya kwanza au Uzamili, Chuo
alichosoma shahada ya kwanza, kiwango cha ufaulu katika shahada ya
kwanza kuanzia GPA 3.0 na Uwiano wa jinsia.
Faida
ambazo Tanzania itapata kutokana na ufadhili huu ni kuongeza wataalam
katika fani za sekta za nishati na madini na hasa sekta ndogo ya mafuta
na gesi, kuongeza fursa za masomo kwa watanzania hasa kwa kuzingatia
kuwa wengi hukosa elimu kutokana na kutomudu gharama, na kuzidi
kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na China.
No comments:
Post a Comment