Picha ya pamoja kati ya wachezaji na mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa
Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa
Mashindano hayo, Emmanuel John Mashindano ya Mbagala Cup
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya
Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke
(MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John
wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya
Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke
(MNEC), Phares Magesa akikabidhi zawadi ya jezi na mpira kwa washindi.
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya
Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke
(MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John
na wageni wa meza kuu wakifuraia jambo
Kaimu
Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye
pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa
akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye
pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa
akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi. Kushoto ni Mlezi wa
Mashindano hayo, Emmanuel John Mashabiki wa Que Bac washindi wakiwa wamembeba goli kipa wao wakishangilia. mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) akikabidhi zawadi kwa golikipa bora.
Mchezaji bora akipokea kitita cha shilingi laki moja toka kwa mgeni
rasmi Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka
ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke
(MNEC), Phares Magesa
Timu
kapteni wa Kipati akikabidhiwa zawadi ya timu yao na mgeni rasmi.TIMU ya
Vijana ya Mpira wa Miguu ya Que Bac ya Mbagala Kipati jijini Dar es
Salaam jana imeibuka bingwa wa Mashindano ya Mbagala Cup baada ya
kuibugiza timu ya mpira wa miguu ya Kipati magoli 2 kwa bila.
Que
Bac imetawazwa mabingwa na kukabidhiwa Mbuzi, seti moja ya jezi pamoja
na mpira.
Que Bac ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Kipati ndani ya
dakika 45 za kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji wao hatari, Yahya
Tumbo (9) alikwamisha mpira katika nyavu za wapinzani baada ya
kuunganisha pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake.
Lakini
hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Que Bac walikuwa mbele kwa goli
moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo wachezaji wa Kipati waliongeza
mashambulizi kwa wapinzani wao kutaka kusawazisha goli lakini goli kipa
wa Que Bac pamoja na walinzi wake walikuwa makini na kuondoa hatari
zote mara kadhaa langoni mwao.
Jahazi
la Kipati lilizamishwa zaidi na mshambuliaji wa Que Bac, Shine Duu jezi
namba 17 ambaye alifanikiwa kuifungia timu yake goli la pili na
kuongeza matumaini ya kutangazwa Mabingwa wa Mashindano hayo (Mbagala
Cup).
Hadi
kipenga cha mwisho Que Bac 2 na Kipati 0.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa fainali, Mratibu wa Mashindano hayo,
Musa Hemed (Kibwetele) alisema mashindano hayo yalianza rasmi Aprili 5,
2014 ambapo timu 16 zilishiriki katika mashindano huku zikiwa katika
makundi mawili, yaani A na B na kila kundi lilikuwa na timu nane.
Alisema
mshindi wa pili katika mashindano hayo amefanikiwa kupata seti moja ya
jezi pamoja na mpira, huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwa wachezaji na
timu yenye nidhamu.
Alisema lengo la mashindano hayo ilikuwa kuwakuza vijana katika vipaji
vyao kwenye fani ya mpira wa miguu pamoja na kuwaunganisha vijana
kushiriki katika michezo kwa pamoja.
"...Sisi
eneo letu tumezoea kuona mashindano ambayo yanaanzishwa labda na diwani
lakini tena mara moja kwa muda mrefu. Sasa mimi nikakaa na kufikiria
nasie vijana tunaweza kujipanga na kuanzisha mashindano kama
hayo,...nikazialika timu tukachangishana ada kidogo na hatimaye tukapata
mlezi wa mashindano na yamefanyika," alisema Kibwetele.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi zawadi, mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa
ni Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari
(TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares
Magesa ameahidi kuyafadhili mashindano hayo kuanzia sasa na atakuwa
akiwezesha kufanyika kwake.
Mbali
na kiongozi huyo kuyafadhili liongeza zawadi kwenye mashindano hayo
ambapo alitoa shilingi laki moja moja kwa mchezaji bora, kipa bora na
waamuzi na kamati ya maandalizi wa mashindano hayo.
Naye
Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John alisema lengo la mashindano hayo
ni kutaka kuwaleta vijana karibu, kuleta upendo dhidi yao na kudumisha
umoja na amani kwa vijana wote.
Alisema
mashindano kama hayo yanawatoa vijana kutoka katika mtizamo ya wao
kukaa vijiweni na kujishughulisha na michezo zaidi ambayo inamanufaa
kwao kuliko kushinda wakipiga soga kwenye makundi vijiweni. Zimeshiriki
Kata tano za Kata ya Mbagala, Kata ya Kiburugwa, Kata ya Kijichi,
Mbagala Kuu
"Unajua vijana wengi mitaa yetu wanakaa vijiweni si kwamba wanapenda
kufanya hivi, wanafanya tu kwasababu wanakosa cha kufanya...sasa kuna
kila sababu watu wenye nafasi kujitokea na kuwawezesha ili kuwatoa
walipo, nimetokea mimi nimedhamini mashindano yamefanyika, wameshindana
na vijana wamepata burudani, upendo na amani pia mshindi kapatikana,"
alisema.
Aidha
alisema wapo vijana wengi wenye vipaji ambao wanaitaji kupewa nafasi za
kushiriki katika mashindano kama hayo na hatimaye vipaji vyao kuonekana
na kuendelezwa katika mashindano ya juu.
"...Tumeona
leo hapa vijana wameondoka na zawadi mbalimbali wachezaji bora
wamezawadiwa, timu bora, golikipa bora kapatikana, timu zimejishindia
jezi na mipira vyote vyao...timu hizi awali zilikuwa zikicheza na jezi
za kukodisha lakini leo wamepata za kwao baada ya kushinda," alisema.
Kijana
huyo alisema anajivunia kuwa sehemu ya kupunguza maovu kwa vijana kwani
katika kipindi chote cha mashindano hayo vijana walielekeza nguvu zao
nyingi kwenye michezo kimashindano jambo ambalo anaamini limepunguza
baadhi wenye nia ovu kubadili mienendo yao kutokana na mashindano hayo.
Pamoja
na hayo aliishauri Serikali na vyama vya soka kushuka ngazi ya chini
mitaani kusaka vipaji vya michezo anuai kwani zipo vingi lakini vinakosa
fursa ya kuonekana.
No comments:
Post a Comment