Naibu
Waziri wa Nishati ametajwa kwenye njama za kutaka kumuua Katibu mkuu wa
CHADEMA Dr. Slaa pamoja mbunge wa Ubungo John Mnyika kwa kuilipua
Helikopta wanayosafiria.
Magazeti ya Tanzania August 9 2014 kama Tanzania Daima na Nipashe
yameripoti kwamba Naibu Waziri huyo anadaiwa kupanga njama za kuilipua
Helikopta ya Dr. Slaa na Mnyika wakiwa ziarani mkoani Shinyanga
kukusanya maoni ya Wananchi juu ya muundo wa serikali mkoani Shinyanga.
Tuhuma
hizo zilitolewa na diwani wa kata ya Ngokelo Sebastian Peter kutoka
Shinganga ambae anasema yeye na mwenzake Zakaria Mfukwa waliahidiwa
shilingi milioni 180 kila mmoja kwa ajili ya kuikamilisha hiyo kazi na
walipewa kazi hiyo ya kutoa taarifa zote kuhusu kutua kwa Helikopta hiyo
na kazi ya ulipuaji ingesimamiwa na Waziri mwenyewe ambayo hata hivyo
haikufanikiwa.
No comments:
Post a Comment