Na mwandishi wetu,Arusha
Shule ya Msingi Levolosi inakabiliwana na changamoto ya ukosefu wa bwalo la wanafunzi kulia chakula nakulazimika kupata huduma ya uji wakiwa
madarasani au wakati mwingine nje mazingira ambayo si mazuri kiafya.
Mkuu wa Shule ya Msingi Levolosi, Elisante Kaaya amesema kuwa wamekua wakikosa
sehemu maalumu ya wanafunzi kujipatia chakula na kueleza kuwa changamoto nyingine
wanazokutana nazo ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia Teknolijia ya habari na mawasiliano(Tehama).
Akisoma taarifa
ya Shule hiyo katika uzinduzi wa jiko la
shule, lilojengwa kwa msaada wa mfanyabiashara Daniel Materi ikiwa ni
njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za kufanikisha mpango wa chakula mashuleni.
Elisante
Kaaya amewapongeza wadau wote waliojitoa kuwezesha watoto wa shule hiyo kupata uji
kwani mwakani wanatarajia watoto watapata huduma ya chakula cha mchana shuleni
hapo.
Mbunge wa
Simanjiro mkoa wa Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema kuwa ni jukumu la jamii kujitoa kusaidia watoto
waweze kusoma na kuzingatia taaluma ili waweze kufaulu.
Hata hivyo mkuu
wa wilaya ya Arusha, John Mongela alihimiza juhudi nzuri zilizofanywa na mfanyabiashara huyo ziigwe na wengine kwani serikali pekee yake haitaweza kutoa zote kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi.
Daniel
amesema kuwa msaada huo ni mchango wa kuisaidia jamii inayomzunguka hususani
katika masuala ya elimu ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.
No comments:
Post a Comment