Meneja Masoko wa Kampuni ya Mbegu ya Seed Co ya jijini Arusha,Frank Wenga(kulia)akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari leo,kushoto ni Meneja Mauzo,Daniel Mwambugi. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
KAMPUNI
YA SEED CO KUZAWADIA WANAFUNZI MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA MIL 15 KATIKA
SHINDANO LA MASHAMBA DARASA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.
Kampuni
ya Seed Co Tz Ltd imezindua rasmi shindano la mashamba darasa kwa shule za
Msingi Tanzania ambapo shule itakayokuwa
imelima shamba zuri kwa kuzingatia misingi yote ya kilimo bora cha kisasa
itajishindia zawadi kubwa ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15
za Kitanzania.
Shindano
hili ni mahsusi kwa shule za msingi zilizopo katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo
ni Kagera, Kigoma, Tabora, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Mara.
Hii
ni baada ya kugundua kuwa ukiachia mbali juhudi za serikali katika kukifanya
kilimo kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu, changamoto kubwa bado imebaki kuwa katika
elimu ya somo hili. Na ndio maana kampuni ya Seed Co ikaona kuwa kama tunataka
kufikia malengo haya basi juhudi kubwa inatakiwa iwe katika kufundisha
Watanzania kilimo kwa njia ya vitendo kwa kuanza kufundisha wanafunzi wa shule
za msingi na kuwapa motisha ya kujishindia zawadi kemkem kutoka Seed Co.
Ukiachia
mbali zawadi kuu ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15 za
Kitanzania, zawadi nyingine zitakuwa ni sare za michezo, vibao vya kuandikia,
madaftari na kalamu za kuandikia. Bila kusahau kuwa mwalimu wa somo la kilimo
ambaye ataifanya shule yake ishinde atazawadiwa pia simu ya kisasa ya mkononi.
Ili
kushiriki, wanafunzi au walimu wanatakiwa kutembelea maduka ya mawakala
waliothibitishwa wanaouza mbegu za Seed Co au kununua gazeti la Nipashe toleo
la kesho tarehe 13 Agosti 2014 ambapo watajipatia nakala yenye tangazo au fomu
ya kujiunga na shindano hili. Kumbuka mwisho wa kujisajili kwa shindano hili ni
tarehe 30 mwezi Agosti 2014.
Katika
uandaaji na usimamizi wa mashamba darasa haya, kampuni ya Seed Co itatoa pembejeo zote
zinazohitajika, ikiwa ni mbegu za mahindi, mbolea ya kupandia na kukuzia na pia
madawa ya kupulizia iwapo mazao yataonyesha dalili za kushambuliwa na wadudu
waharibifu.
Kumbuka
ya kwamba kampeni hii ya Mashindano ya Mashamba Darasa imelenga kufundisha
Kilimo kwa njia ya vitendo kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, huku ikitoa nafasi
kwa wanafunzi kujishindia zawadi mbali mbali kutoka Seed Co. Zawadi kuu ni
kushinda Madawati 100 yenye thamani ya
shilingi Milioni 15 za Kitanzania. Hii ni motisha kubwa kwa wanafunzi
kupenda shughuli za kilimo tangu wakiwa shuleni.
Kuhusu Seed Co
Seed Co Limited ni kampuni inayoongoza barani Afrika kwa kukuza, kuzalisha, kubangua
na kusambaza mbegu bora katika masoko ya nchi 15 barani Afrika. Bidhaa nyingi
za mbegu zinazozalishwa na kampuni hii ni pamoja na mahindi, Pamba, Ngano, Soya, Mtama na mazao mengine ya
nafaka ndogondogo.
Katika soko la Tanzania Seed Co imejikita zaidi katika uzalishaji wa mbegu chotara za mahindi na mtama. Kampuni hii kwa sasa ina viwanda vya kubangua mbegu Jijini Arusha na Mbeya. Jijini Mwanza kuna ghala kubwa la kuhifadhia mbegu ikiwa ni mkakati wa kumfikishia mkulima bidhaa hizi karibu naye.
Katika soko la Tanzania Seed Co imejikita zaidi katika uzalishaji wa mbegu chotara za mahindi na mtama. Kampuni hii kwa sasa ina viwanda vya kubangua mbegu Jijini Arusha na Mbeya. Jijini Mwanza kuna ghala kubwa la kuhifadhia mbegu ikiwa ni mkakati wa kumfikishia mkulima bidhaa hizi karibu naye.
No comments:
Post a Comment