Lango
kuu la kuingilia katika Shule ya Msingi na Awali ya Sunrise iliyopo
jijini Dar es Salaam likiwa na maandishi ya kukaribisha wageni katika
mahafali ya Saba ya Shule hiyo yaliyofanika jana.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa
Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya maua kutoka kwa wanafunzi wa
Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam wakati
alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Saba ya wahitimu wa Darasa la
Saba jana.
Mwanafunzi
anayehitimu Darasa la Saba katika Shule ya Msingi na Awali Sunrise Bw.
Mark Ngalo akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake wakati wa
mahafali yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.Aliyemshikia kipaza
sauti ni Lulu Benson.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na M,ichezo Profesa
Elisante Ole Gabriel akizungumza na wazazi na wanafunzi wakati wa
mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi na Awali
Sunrise ya jijini Dar es Salaam jana alipokuwa mgeni rasmi katika
mahafali hayo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na M,ichezo Profesa
Elisante Ole Gabriel akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Darasa la
Saba katika Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam
wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Saba ya Shule hiyo
yalifanyka jana jijini Dar es Salaam. Katika ni Mwalimu Mkuu wa Shule
hiyo Mwalimu Onesmo Vitalis.
Kikundi
cha Skauti cha Shule ya Msingi na Awali Sunrise wakitoheshi mbele ya
mgeni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (hayupo pichana) alipokuwa mgeni
rasmi katika mahafa ya saba kwa wahitimu wa Darasa la Saba katika shule
hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Awali ya Sunrise wakifurahia kwa
michezo wa sanamu wakati mahafali ya darasa la Saba jana jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wahitimu wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya
jijini Dar es Salaam wakiwa wenye nyuso za furaha wakati wa mahafali yao
jana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment