Pages

August 22, 2014

Mh. Kigoda afungua maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China jijini Dar


Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda na Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Shenzhen Yingli New Energy Resources Honglin Hui (Kulia) akimueleza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (kushoto) jinsi Solar Panel inayotengenezwa na kampuni hiyo inavyofanya kazi wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China yaliyofunguliwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia pikipiki aina ya SWAN inayotengenezwa na kampuni ya Honda ambayo inayotumia mafuta ya Petrol na Umeme wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China. Kulia kwake ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na kushoto ni Juwes Wang ambaye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia viatu vinavyozalishwa nchini China wakati wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa nchini humo ambayo yamefunguliwa  na kumalizika jumapili ya tarehe 24/8/2014.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia vitenge vinavyozalishwa nchini China wakati wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa nchini humo .
Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing akimkabidhi zawadi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.
Charley Peng kutoka kampuni ya China Wuxi Everbright akimwonyesha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda bajaji aina ya Dudu inayozalishwa na kampuni hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akimsikiliza Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.

Baadhi ya wageni aliohudhuria sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (hayupo pichani) . Picha na Anna Nkinda- Maelezo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...