Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 3.8.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Help for Underserved Communities (HUC) ya nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
Baada ya kutembelea maonesho ya wanawake wajasiriamali Mama Salma Kikwete akifuatana na Afisa Tawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka kwenda kuweka saini kwenye kitabu cha wageni.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni. Aliyesimama kushoto ni Bibi Lily Munanka, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa wana kikundi wa TANO Ladies. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti Asha Hariz, akifuatiwa na Asha Nyang’anyi, Isca Kauga, Juster Mutakyawa na Tumaini Kaisi aliyeshika kipaza sauti.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kikundi cha TANO Ladies cha nchini Marekani. Anayekabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya wanakikundi wenzake Ndugu Juster Mutakyawa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi ya wanawake mwishoni mwa mazungumzo yake na wanawake hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani huko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke wa Rais akipiga picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
Balozi wa Tanzania nchni Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula akimuaga Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kutembelea ofisi za ubalozi huo na kuongea na wanawake wa Tanzania wanaoishi nchini Marekani. PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment