Pages

August 17, 2014

MABORESHO YA USIMAMIZI FEDHA ZA UMMA YANAVYOBORESHA MAISHA


Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Ingiahed Mduma  (wa pili kushoto) na  Kassim Kobelo Mkuu wa Hazina ndogo Mkoa wa Lindi ( wa pili kulia) wakiwa wameshika cheti cha ushindi wa pili wa maonyesho ya Kitaifa  ya Nanenane  yaliyofanyika Ngongo, Mkoani Lindi hivi karibuni.
Mkuu  wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha, Ingiahed Mduma akiwa na baadhi ya watumishi katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yaliyofanyika Ngongo, Mkoani Lindi hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki wa Maonyesho wa Banda la Wizara ya Fedha mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi katika Maonyesho ya  Kitaifa ya Nanenane Ngongo, Mkoani Lindi hivi karibuni.

KATIKA maonesho ya wakulima maarufu kama Nanenane yaliyomalizika hivi karibuni kitaifa mkoani Lindi, Wizara ya Fedha ilishika namba mbili katika taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi nyuma ya Jeshi la Magereza.
Kilichoifanya Wizara hiyo kushika nafasi hiyo ni kutokana na kutoa elimu muhimu kwa wakulima kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu fedha na uchumi wa nchi yetu, pamoja na maboresho ambayo yanaendelea serikalini.
Kila idara, kuanzia kwenye Ofisi ya Mhasibu Mkuu hadi kwenye idara za zinazohusika na pensheni, wananchi, kwa maana ya wakulima, walijifunza mengi kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo wizara hiyo.
Kwa, mfano katika ofisi ya Mhasibu Mkuu, wengi walijua kwamba, kama unafanya kazi serikalini na kutunza kumbukumbu vizuri, unalipwa stahiki zako mapema sana.
Hata hivyo, katika makala haya tunaangalia idara moja wapo ambayo ilitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye maonesho hayo, namna ambavyo  imekuwa ikifanya maboresho mbalimbali katika kusimamia fedha za umma. Hii ni Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP)
Mtu ambaye alifika kwenye idara hiyo, aligundua mengi ikiwa ni pamoja na mchango wa PFMRP katika ujio na utendaji madhubuti wa sasa wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ujio wa Mamlaka ya Uthibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na kwamba mkakati unafanywa katima kuhakikisha serikali za mitaa zinapunguza utegemezi wa kibajeti kwenye serikali kuu kwa kuweza kukusanya mapato makubwa zaidi. Kwa sasa serikali hizo zinakusanya kati ya asilimia 10 na 12 pekee.
Hii programu ni nini?
Serikali kwa kipindi cha kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 imekuwa ikitekeleza kwa awamu Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP).
Lengo la programu hii bu kudhibiti na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika Serikali na taasisi zake. 
Mafanikio yamepatikana katika maeneo ya kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani, udhibiti wa madeni, kutumika kwa mipango ya muda wa kati; usimamizi wa misaada na fedha za washirika wa kimaendeleo, uwazi katika kutathmini matumizi ya umma, mapitio ya sheria na miongozo ya usimamizi wa fedha, ununuzi na ugavi wa rasilimali za umma.
Awamu ya kwanza hadi ya tatu
Awamu ya kwanza ya programu hii ya kuanzia mwaka 1998 hadi 2004 ililenga kudhibiti matumizi ya Serikali, kuhakikisha kuwepo kwa nidhamu ya mapato na matumizi ya Serikali na kuchangia katika kukuza uchumi endelevu
Awamu ya Pili iliyoanza mwaka 2004 hadi 2008 ililenga kuboresha taratibu na mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kwa kutumia viwango vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha rasilimali zinatengwa kimkakati katika maeneo ya vipaumbele.
Awamu ya Tatu iliyojiri kati ya mwaka 2008 na 2012 ilikuwa ilijielekeza katika kuhakikisha kuwa, mbinu na mifumo iliyowekwa katika awamu ya kwanza na ya pili inaoanishwa na kutumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa
Usimamiaji Fedha Awamu ya Nne
Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Nne  ndio tunayoendelea nayo hadio sasa. Utekelezwaji wake ni kuanzia kipindi cha mwaka wa fedha 2012/13 hadi 2016/17.
Lengo la awamu ni kuhakikisha kunakuwa na  nidhamu katika Usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa Umma ili kuleta Maendeleo Endelevu
Maeneo ya kuboresha
Eneo la Kwanza la kuboresha ni usimamizi wa Mapato. Eneo hili linahusu kuboresha makadirio na ukusanyaji wa mapato na kuhuisha Sera, Sheria na Kanuni za Mapato.
Matokeo yanayotarajiwa ni kuimarisha mifuo, michakato na taratibu kwa ajili ya kuboresha uweza wa utendaji wa ukusanyaji wa mapato.
Eneo la pili ni Mpango na Bajeti ambapo linalenga kuboresha sera za fedha, mipango, bajeti ya muda wa kati na kuanzishwa kwa mpango na bajeti ya kiprogramu (programme based budgeting).
Eneo hili litazingatia pia uboreshwaji wa takwimu za kibajeti (GFS Codes 2001) na uchambuzi wa shughuli za Serikali (CoFoG).
Matokeo yanayotarajiwa ni kuimarisha uwezo wa kupanga na usimamizi wa bajeti, ikiwa ni pamoja na matokeo na bajeti za kipgoramu ndani ya Wizara ya Fedha, idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Serikali za Mitaa.
Eneo la tatu ni la utekelezaji wa bajeti, uwazi na
uwajibikaji.
Eneo hili linalenga kuhakikisha uhalisi wa maoteo ya bajeti ya matumizi, kuboresha uwezo wa ununuzi, usimamizi wa fedha na madeni na kupanua wigo, utunzaji na utoaji bora wa taarifa za fedha.
Matokeo yanayotarajiwa ni kuboresha matumizi ya rasilimali za umma kwa njia bora zaidi, ufanisi na uwazi.
Eneo la nne ni usimamizi na udhibiti wa bajeti. Eneo hili linahusisha kutoa miongozo ya kiutaalamu na kujenga uwezo kwa wizara na idara zinazojitegemea sambamba na Wakala wa Serikali, Sekretariati za mikoa na Serikali za Mitaa katika maeneo ya ukaguzi wa ndani.
Matokeo yanayotarajiwa ni Kuboresha Usimamizi na utekelezaji wa udhibiti wa ndani wa fedha, kanuni, sheria, taratibu na mapendekezo ya ukaguzi katika Wizara, idara zinazojitegemea, Wakala wa serikali, Sekretariati za mikoa na Serikali za Mitaa.
Eneo la tano linajielekeza katika usimamizi wa mabadiliko, ufuatiliaji wa program na nawasiliano.
Eneo hili linahusika na masuala mtambuka katika maeneo ya mabadiliko ya menejimenti, uongozi, uratibu, ufuatiliaji, mawasiliano kwa wadau wote na muingiliano wa mifumo ya fedha ambayo ni muhimu kwa utekelezaji wa program.
Matokeo yanayotarajiwa ni kuboresha usimamizi na kuongeza uwajibikaji katika uongozi ili kusimamia vizuri utekelezaji wa program.
Usimamizi wa programu awamu ya nne utafanyika kupitia yafutayo:
Mosi ni kamati ya pamoja (Joint Steering Committee) ambayo itatoa mwongozo wa kimkakati, kupitia na kuidhinisha Mpango na Bajeti na Mpango kazi, na kufuatilia utekezaji wa programu.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Programu ambayo inawajibika katika kuchambua mipango na bajeti, taarifa za utekelezaji zilizoandaliwa, kupitiwa na kukubaliwa na Jopo la Utandaji la Watalamu kabla ya kuwasiliashwa kwenye Kamati ya Pamoja.
Tatu ni Japo la Utendaji la Watalaamu ina maamuzi juu ya masuala ya kitaalam na kutoa mapendekezo kwa Kamati ya Utekelezaji ya Programy na mapitio ya utekelezaji wa programu
Mafanikio ya programu
Baadhi ya mafanikio ya programu yaliyopatikana katika awamu zilizopita pamoja na kuanishwa kwa Sheria ya Ukaguzi wa Umma Namba 11 ya mwaka 2008 ambayo imeimarisha kazi ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Sheria hii imemuongezea uhuru Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi kwa ufanisi zaidi na hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Pili ni marekebisho ya Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 yaliyofanyika mwaka 2010. haya yaliwezesha kuanzishwa kwa Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Marekebisho hayo pia yalimpa mamlaka Mlipaji Mkuu wa Serikali na Mhasibu Mkuu wa Serikali kusimamia na kufuatilia fedha za Mamlaka za Serikali, hivyo yameruhusu kufanya malipo ya Serikali kwa mtandao (Electronic Funds Transfer).
Mafanikio mengine ni Mtandao wa malipo wa Serikali (IFMS) ulioanzishwa kwa ajili ya kusaidia kuthibiti Matumizi ya fedha za umma na kusaidia kuandaa taarifa za fedha.
Nne, taasisi za umma zimejengewa uwezo wa kufanya ununuzi kwa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa umma ya mwaka 2004.
Tano, mpango Mkakati wa Muda wa Kati, Mwongozo wa Bajeti na mfumo wa maandalizi wa matokeo ya bajeti na mgawanyo wa rasilimali katika maeneo yenye vipaumbele (SBAS) vilianzishwa.
Sita, takwimu za kibajeti za Serikali (GFS code) ziliboreshwa kutoka GFS 1986 kwenda GFS 2001.
Saba, Mfumo wa Ulipaji wa Mishara za Watumishi wa Serikali umeunganishwa katika mikoa yote na hivyo kurahisisha uingizwaji wa kumbukumbu za watumishi katika kila kituo.
Nane, programu hii imewezesha Mkakati wa pamoja wa Misaada kwa Tanzania kuanzishwa ili kuongoza taratibu za misaada na muundo wa mijadala.
Manufaa mengine ya programu hii ni kuanzishwa kwa mfumo wa utoaji wa taarifa za misaada na mikopo ya kigeni ili kuwezesha usimamizi na ufuatiliaji.
Changamoto
Si rahisi kuanzisha programu kama hii na kisha kukoeskana kwa ka changmoto. Moja ya changamoto hizo ni kuboresha mapato na Maoteo ya mtiririko wa fedha za serikali kulingana na bajeti ili kutekeleza vipaumbele.
Pili ni kuimarisha utendaji wa mifumo ya usimamizi wa fedha za umma katika ngazi ya Serikali za Mitaa. Tatu, ni linganifu na mahusiano ya mifumo (harmonization of Systems).
Nne ni kuongeza idadi ya wataalamu na uwezo wa kiutendaji na hasa katika usimamizi wa Mikataba na Miradi na changamoto ya tano ni kuweka uwiano mzuri kati ya matumizi ya Maendeleo na matumizi ya kawaida; na kuwa na mfumo madhubuti wa kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa Serikali. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...