Binti huyo akidhibitiwa na polisi.
watoto!
Wanafunzi wawili, wa kike ana miaka 14 (darasa la saba), wa kiume miaka
15 (kidato cha kwanza) mjini hapa wanadaiwa kukutwa ndani ya gesti moja
ikisemekana walikuwa na lengo la kuivunjilia mbali amri ya sita ya
Mungu.Tukio hilo lililojaza umati lilijiri hivi karibuni katika gesti
hiyo ambayo inadaiwa haina usajili halali iliyopo jirani na soko. Habari
zinasema kuwa, siku hiyo denti wa kike alitumwa sokoni na mama yake
kununua mahitaji mbalimbali ya chakula lakini alichelewa kurudi.
Ikazidi
kudaiwa kuwa mama yake alimfuatilia huku akiwauliza watu, ndipo mbeya
mmoja akamtonya kuwa amemwona binti yake akiingia gesti hiyo na
kivulana! Mama wa watu, akiwa na mshangao, naye alizama ndani na
kuwakuta chumba namba 5. Kikanuka!
Risasi
Jumamosi lilifanikiwa kutinga eneo la tukio wakati wa sekeseke hilo na
kuzungumza na mashuhuda wawili, Asha Chande na Tausi Omary.Walipohojiwa
na mwandishi wetu walisema waliwaona wawili hao wakizama ndani ya gesti
hiyo na walishangaa kwa nini walikubaliwa kwa vile wote ni watoto.
...Akizidi kudhibitiwa baada ya kuleta ukorofi.
”Baada ya
muda mama mmoja mtu mzima alifika hapa akiwa amefura kwa hasira,
akadai binti yake aliyemtuma sokoni ameingia gesti, mara na yeye
akaingia ndani, alimkuta yupo na mvulana huyo huku mfuko aliotumwa nao
sokoni binti wa kike ukiwa chini ya kitanda.
“Aliwafurumusha,
kivulana kimekimbia zake na huyu binti ndiyo kama hivi. Mbaya zaidi
hapa ni sokoni, watu wameacha biashara na kujaa,” alisema Tausi.
Wakati
sakata hilo likiendelea, baadhi ya watu walitaka kumwangushia kipondo
denti huyo wa kike kwa kitendo chake cha kuacha alichotumwa na kuzamia
kwenye mapenzi akiwa bado mwanafunzi.
Baadaye
polisi wa pikipiki walifika na kumchukua denti huyo kwa lengo la
kumuokoa na kipigo na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro ambapo
ilidaiwa kuwa polisi walishauri wazazi wa watoto hao wakayamalize
nyumbani.
Juhudi za mwanahabari wetu kutaka kuzungumza na mlinzi wa gesti hiyo ziligonga mwamba baada ya muda mwingi kufunga geti kubwa.
No comments:
Post a Comment