Pages

July 28, 2014

WAZIRI MAHENGE AKIFUTIA VIBALI VYA KUNUNUA KUNI NA MAGOGO KIWANDA CHA SUNFLAG TANZANIA LTD ARUSHA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYVIKdacwqaCswv00Uoce5yqad8UCkU7o9R3ZAfddf90n6A3MgCnaK2CiGg4EtOTMZRpYIuGWA3imQZja9mxQ21Mf_ExDKMJ-GEJU2oWYDcYC2eMkx0GpSxZBz3HRHMMQ6_J40ekYLKd0/s1600/RUNDO+LA+VIPANDE+WA+MAGOGO+KIWANDANI.2.JPG Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imesitisha vibali vyote vilivyotolewa vya kununua kuni na magogo kwa ajili ya nishati ya kuendesha viwanda mbalimbali nchini na badala yake imevitaka ndani ya muda wa miezi mitatu kuanzia leo viwe vinatumia teknolojia ya makaa ya mawe, umeme na gesi kwa ajili ya kuendeshaji wa viwanda hivyo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Dkt Binilith Mahenge baada ya kufanya ziara kiwanda cha kufuma nguo cha Sunflag Tanzania ltd, kilichopo eneo la Themi jijini Arusha na kushutushwa na shehena kubwa ya magogo yaliyorundikwa katika kiwanda cha Sunflug ambayo kiwanda hutumia kwa ajili ya nishati.



” Hali hii inatisha sana katika suala la mazingira na kamwe serikali halitalivumilia kwa kiwanda kama hiki kukata miti kwa kiwango kikubwa hicho na huu ni uharibifu mkubwa wa mazingira “alisema waziri mahenge

Kufuatia hali hiyo Waziri Dkt Mahenge amefuta vibali vyote vilivyotolewa kwa kiwanda hicho kwa ajili ya kununua kuni kwa ajili ya Nishati .


Hali hiyo ya kutisha ya kuwepo na shehena ya magogo Serikali imeuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuacha mara moja matumizi ya nishati ya magogo kuanzia sasa na imetoa muda wa miezi mitatu kiwanda kiwe kimeaanza kutumia nishati ya gesi, umeme na makaa ya mawe.

Ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kinawalipa walinzi watakaowekwa na serikali ngazi ya mkoa ili kuzuia uingizwaji wa magogo na kuni kiwandani hapo kwa ajili ya nishati.


Katika hatua nyingine waziri amekitoza faini ya shilingi milioni 80 kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira ,na kukiagiza kushirikiana na mkoa pamoja na baraza la taifa la mazingira kanda ya kaskazini kutafuta eneo litakalopandwa miti milioni 7 .

Waziri amezitaja sababu mbali mbali zinazosababisha afrika kuendelea kuwa maskini kuwa ni pamoja kuwa tuko nyuma katika matumizi ya sayansi na teknolojia, hatuna elimu kubwa ya kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo njaa na mafuriko yanayoharibu miundo mbinu ,kiwango kikubwa cha uharibifu wa mazingira ,mabadiliko ya tabia nchi, hivyo mkazo zaidi unawekwa kupunguza matumizi ya kuni na badala yake kusisiotiza matumizi ya sayansi na teknolojia.


Waziri huyo wa Mazingira ambaye pia ni mbunge wa makete mkoani Njombe amesisitiza kuwa matumizi ya nishati ya magogo katika uendeshaji maboila katika kiwanda umepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya Teknolojia

Hali hii imeshutua sana waziri Mahenge baada ya kuona shehena kubwa ya magogo hayo ambayo inaaminika yamevunwa kwa kipindi cha miaka mingi ambapo kila siku kiwanda hicho hutumia tani zaidi ya 1,500 za magogo kama nishati.

Akizungumza wakati wa ziara ya kiwanda hicho Mkurugenzi Mkuu wa baraza la taifa la mazingira katika ofisi ya Makamu wa Rais Eng.Boneventura Baya amesema hali hii ni mbaya na haikubaliki kabisa imechangia kwa kiwango kikubwa katika uharibifu wa mazingira.

Amemwagiza Mwanasheria wa Baraza la taifa la mazingira ,Machale Heche kuchukua hatua za haraka kuanzia leo kusimamisha uingizaji wa magogo katika kiwanda hicho na kusisitiza kuwa kuanzia jana hakuna mzigo au shehena ya aina yeyote ya kuni na magogo itakayoingizwa kiwandani hapo na oda zote zilizokuwa zimetolewa na kiwanda hicho za ununuzi wa kuni na magogo zimesimamishwa.

Mhandisi Baya alisema kiwanda hicho kimekuwa kikivuna miti ya asili na ile ya kupanda hali ambao imechangia uharibifu mkubwa wa mazingira.

Amesema magogo yamevunwa kwa zaidi ya miaka saba hivyo ameonya kwamba tuogope kuchezea suala la mazingira.

Kwa upande wake Mwanasheria katika baraza la Mazingira la taifa Manchale Heche amesema kutokana na shehena kubwa ya miti iliyovunwa na kiwanda hicho uongozi wa kiwanda hicho unapaswa kupanda zaidi ya miti milioni saba ili kufidia uharibifu huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...