Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya Vulcan ya nchini Marekani
Bw. Dave Stewart (kushoto) na Bi. Lauren Ryder, inayojihusisha na
masuala ya kuidadi tembo katika nchi 18 barani Afrika ikiwemo Tanzania,
baada ya kufanya mazungumzo maalum ya ushirikiano yaliyofanyika katika
jiji la New York nchini Marekani jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiagana na Bw. Dave
Stewart kutoka Taasisi ya Vulcan inayojihusisha na masuala ya kuidadi
tembo katika nchi 18 barani Afrika ikiwemo Tanzania mara baada ya
kumaliza mazungumzo nao jana jijini New York nchini Marekani.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza na Balozi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi mara
baada ya kukamilika kwa kikao jana baina ya Waziri Nyalandu na ujumbe
wake pamoja na taasisi mbalimbali za uhifadhi jijini New York, Marekani.
Kati ni Katibu wa Waziri Bw. Imani Nkuwi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (watatu kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya inaundwa na
Wanajeshi Wastaafu wa jeshi la Marekani walioanzisha umoja wao
ujulikanao kama (VETPAW)kwa ajili ya kusaidia Uhifadhi wa Wanyamapori
barani Afrika mara baada ya kumaliza mazungumzo baina yao jana jijini
New York, Marekani. Kushoto ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa
Mataifa Balozi Tuvako Manongi.
No comments:
Post a Comment