Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI)Isaya Mngulu akishauriana na maafisa wake leo |
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI)Isaya Mngulu |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya saa
22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la
Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi. Kufuatia uchunguzi huo kati
yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni:
1. SHAABAN
MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26
Kabila, Msambaa. Mlinzi aliyekuwa
zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
2. ATHUMAN HUSSEIN MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa,
Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la
tukio.
3. MOHAMED NURU @ MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila
Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani na eneo la tukio.
4. JAFFAR HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa
Shule ya Msingi Olturmet Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA
mjini Arusha. Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko
ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
5. ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa
Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi
Arusha.
6. SAIDI
MICHAEL TEMBA; umri wa miaka 42,
Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku maeneo
ya Sombetini walikamatwa YUSUFU HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa
miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA , kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani
kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi
sita za shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo
na bisibisi moja. Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa
wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha. Mahojiano
yanaendelea dhidi yake.
Uchunguzi wa shauri hili pamoja na matukio mengine
ya milipuko unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi
mwa Polisi na kuwakamata watakao bainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa
matokeo ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila mrangi,
umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo la Chemchemu
Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini.
Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji
wa mhalifu huyu.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa
ushirikiano mkubwa wanaoutoa. Asanteni.
………………...…………..
ISAYA MNGULU-CP
MKURUGENZI WA
UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA
No comments:
Post a Comment