UJERUMANI
imetinga Fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuwafumua wenyeji, Brazil
mabao 7-1 katika mcheo wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Mineirao
mjini Belo Horizonte, Brazil.
Ujerumani
inaingia Fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12- mara ya mwisho
ilifungwa na Brazil katika fainali zilizoandaliwa kwa pamoja na Korea
Kusini na Japan na sasa watamsubiri mshindi wa kesho kati ya Argentina
na Uholanzi.
Hadi
mapumziko, tayari Ujerumani walikuwa mbele kwa mabao 5-0 yaliyofungwa
na Toni Kroos mawili, Miroslav Klose, Thomas Muller na Sami Khedira.
Brazil ilionekana wazi kuathiriwa na pengo la kuwakosa wachezaji wake
tegemeo, beki na Nahodha Thiago Silva anayetumikia adhabu ya kadi za
njano na mshambuliaji Neymar ambaye ni majeruhi, ambao nafasi zao
zilizibwa na Bernard na Dante.
Ujerumani ilipata bao lake la kwanza dakika ya 11, mfungaji Thomas Muller baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Brazil.
Miroslav Klose akafunga la pili
dakika 23 baada ya kuukuta mpira uliopanguliwa na kipa Julio Cesar
kufuatia shuti lake mwenyewe na kuandika bao lake la 16 kwenye Fainali
za Kombe la Dunia akiweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi
zaidi kwenye fainali hizo, akimpiku Mbrazil, Ronaldo Lima.
Toni Kroos akaifungia Ujerumani bao la tatu na la nne dakika za 24 na 26, kabla ya Sami Khedira kufunga la tano dakika ya 29.
Kipindi cha pili, kocha wa
Brazil, Luiz Felipe Scolari alianza na mabadiliko, akiwatoa Fernandinho
na Hulk na kuwaingiza Paulinho na Ramires, wakati mwenzake wa Ujerumani,
Joachim Loew alimpumzisha Hummels na kumuingiza Mertesacker.
Mabadiliko hayo kidogo
yaliiongezea uhai Brazil na kupeleka mashambulizi langoni mwa Ujerumani,
lakini wakaishia tu kukosa mabao ya wazi.
Ujerumani ikafunguka tena na
kwenda kufunga mabao mawili zaidi, yote Andre Schurrle aliyeingia dakika
ya 58 kuchukua nafasi ya Klose akimtungua kipa Julio Cesar dakika ya 69
na 79.
Brazil ilianya tena mabadiliko,
Fred akimpoisha Willian dakika ya 69, wakati Ujerumani nayo
ilimpumzisha Khedira nafasi yake ikachukuliwa na
Draxler dakika ya 76.
Mesut Ozil alipata nafasi nzuri
ya kufunga dakika ya 89, lakini akapiga nje na Brazil wakafanya
shambulizi na kushitukiza na kujipatia bao la kufutia machozi
lililofungwa na Oscar dakika ya 90.
Wachezaji na mashabiki wa Brazil waliangua vilio baada ya mchezo huo, huku Wajerumani wakiangusha pati la maana uwanjani
No comments:
Post a Comment