Rais
Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na David Shambwe Kulia Mkurugenzi wa
Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC) na Felix Maagi Kaimu
Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo, Wakati
alipowasili katika banda la (NHC) na kukagua, Kupata maelezo mbalimbali
ya shughuli za miradi inayotekelezwa na shirika hilo. Wakati
alipotembelea maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (TANTRADE)
maarufu kama Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya
Kirwa jijini Dar es salaam. Yanayofikia tamati kesho jijini Dar es
salaam , Katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa
Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wa pili kutoka kulia ni
Elias Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa
Mawasiliano NHC.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea
banda la Shirika la Nyumba NHC kwenye maonyesho ya Sabasaba Viwanja vya
Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wanaoshuhudia
ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dr. Abdalla Kigoda na Nalindwa
Norbert mmoja wa maofisa wa Shirika la Nyumba NHC.
Baadhi
ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwahudumia watu mbalimbali
waliotembelea banda lao ili kupata maelezo mbalimbali ya shughuli
zinazofanywa na shirika hilo.
Baadhi
ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Yahya
Charahani Meneja Uhusiano wa NHC , Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara
(NHC) Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha
Bw. Felix Maagi , Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki na
Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC).
Baadhi
ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara NHC Bw. David Shambwe , Kaimu
Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi,
Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC) na Yahya Charahani
Meneja Uhusiano wa (NHC) wakisubiri kuwasili kwa Mh. Rais Dr. Jakaya
Kikwete katika banda lao.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akiendelea kupata maelezo kutoka kwa Bw. David
Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC)
wakati alipotembelea banda hilo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
No comments:
Post a Comment