Pages

July 3, 2014

OFISI YA BUNGE YAANDAA MNUSO WA NGUVU KWA MAMENEJA WA HOTELI ZA KITALII JIJINI ARUSHA

Katibu wa Bunge,Dk Thomas Kashililah(kushoto)akisalimiana na Meneja wa Fedha wa Hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa  Mameneja wa Hoteli za kitalii ikiwa maandalizi ya mkutano mkubwa wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola(CPA)utakaofanyika jijini Arusha mwezi huu.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,John Mongela(kulia)akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Mawasiliano,Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge,Jossey Makasyuka wakati wa hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola(CPA)tawi la Tanzania,Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya chakula jioni,wengine kutoka kushoto ni Wabunge wa Vita Maalumu,Mhonga Ruhwanya,Lucy Owenya,Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete na Mbunge wa Kilindi,Beatrice Shelukindo.

Wakifatilia kwa makini hafla hiyo,kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha AICC,Paul Ndosa,Wabunge  wa Viti Maalum,Mhonga Ruhwanya na Lucy Owenya.

Mameneja mbalimbali wakifatilia kwa makini tukio hilo ambalo litawawezesha kupokea wageni  wengi kwenye hoteli zao.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,John Mongela akiwaongoza washiriki wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwaajili ya maandali ya Mkutano wa 45 wa CPA.

Katibu wa Bunge,Dk Thomas Kashililah  akishiriki chakula cha jioni,akifatiwa na Meneja wa Hoteli ya Naura Spring ya jijini Arusha,Beatrice.

Meneja Masoko wa Kibo Palace Hoteli,Charity Githinji hakuwa nyuma kuchangamkia msosi katika hafla ya chakula cha jioni katika hoteli ya Mount Meru.

Meneja  Utawala wa Hoteli za Impala,Laizer Ole Mattasia(kushoto)Mkuu wa Idara ya Mawasiliano,Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge,Jossey Mwakasyuka na Meneja wa Fedha wa Ngurdoto Mountain Lodge,Bonny Tarimo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...