Mwanafunzi (LEMA) aliyejeruhiwa kwa moto |
Mwanafunzi
huyu Daniel Lema alikuwa akisoma mwaka wa nne, kozi ya sheria katika
chuo kikuu kishiriki cha Mt. Augustino cha Ruaha Iringa (Ruaha
University College maarufu kama RUCO).
Mwanafunzi huyo alichomwa moto wiki iliyopita akihusishwa na tuhuma za wizi.
Baada ya kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa wiki moja sasa, mwanafunzi huyo ameaga dunia majira ya saa nane mchana.
Taratibu za kuaga mwili wake zinaendelea kufanywa na uongozi wa chuo hicho, ndugu na wanafunzi wenzake.
Taarifa
za awali zinaonesha kwamba mwili wake utaagwa kesho kuanzia saa moja
asubuhi kabla ya kusafirishwa kupelekwa kwao mkoani Kilimanjaro kwa
mazishi. Mazishi ya kijana huyo yanatarajia kufanyika jumatano ya wiki
hii.
Juni 24, mwaka huu Daniel
Lema alikutwa na mkasa wa kukamatwa na kuchomwa moto wakati akitoka
kuangalia fainali za kombe la dunia katika moja ya Bar za mjini Iringa.
Akiwa amelewa aliingia katika moja ya migahawa ya mjini hapa akitafuta chakula, ilikuwa majira ya saa tano mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara hiyo ilikua imefungwa.
Binti
aliyekuwepo katika mgahawa huo alianza kupiga kelele akidhani kavamiwa
na mwizi. Mlinzi wa eneo hilo (mmasai) alimvaa kijana huyo na
kumshambulia.
Baada
ya tukio hilo taarifa zinasema walitokea watu wawili waliojitambulisha
kuwa ni askari; askari hao walizuia watu waliozidi kujitokeza katika
eneo hilo kuendelea kumpiga kijana huyo.
Wakiwa
njiani, wananchi hao waliokuwa wakifuatilia kama atafikishwa kituo cha
Polisi waliona wanachalewa na kuamua kuchukua sheria mkononi kwa
kuendelea kumpiga kabla ya kumchoma moto.
chanzo: http://frankleonard.blogspot.com
No comments:
Post a Comment