Pages

July 24, 2014

Mlipuko wa bomu waua watu 25 Nigeria


Wanamgambo wa kiislamu, Boko Haram wamekuwa wakitekeleza mashambulizi kadha wa kadha ya mabomu na mauaji nchini Nigeria tangu walipoanza Operesheni yao mwaka 2009 wakiwa na nia ya kuunda nchi ya kiislamu. Boko Haram huwashambulia viongozi wa kiislamu ambao hukosoa misimamo yao.
 


Jeshi la polisi nchini Nigeria limetoa taarifa ya kuuawa takriban watu 25 kutokana na mlipuko wa bomu ulio tokea leo jioni katika barabara ya Isa Kaita mjini Kaduna.Bomu hilo lilimlenga Kiongozi wa dini ya kiislamu mwenye msimamo wa wastani Dahiru Bauchi ambaye alikua akitoka kuhubiri katika viwanja vya Murtala Muhammed. Bauchi amenusurika katika shambulio hilo, hajajeruhiwa halikadhalika bado haijajulikana waliofanya shambulio hilo.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...