Wanafunzi
walionusurika katika mkasa wa feri iliyozama nchini Korea Kusini mwezi
Aprili wamesema kuwa waliagizwa kusalia katika vyumba vyao wakati meli
hiyo ilipozama .Walikuwa
wanatoa ushahidi katika kesi inayomkabili nahodha na wafanyikazi wa
meli hiyo wanaokabiliwa na mashtaka ya uzembe na mauaji kufuatia kufa
maji kwa takriban watu 300 katika mkasa huo.
Mwanafunzi
mmoja amesema kwamba yeye na wenzake walifuata maagizo hayo hadi pale
mlango wa chumba chao ulipokuwa juu ya vichwa vyao huku maji yakiingia
ndani ya feri hiyo kupitia madirishani.
Wahudmu walituhimiza tutuliea licha ya kuwa ferry ilikuwa inazama
Wanafunzi wananza kutoa ushahidi Korea
Mwengine alitaka kujua ni kwa nini waokoaji hawakuingia ndani ya chombo hicho ili kuwasaidia kutoka.
Wanafunzi walikaribia kwenye milango ya kutoka ambapo walisaidiwa kutoka na wanafunzi wenzao.
Feri hii ilizama tarehe kumi na sita mwezi wa Aprili kwenye kisiwa cha Jeju ambapo watu mia tatu na wanne waliaga dunia.
Wanafunzi hao walikuwa wakitoa ushahidi katika kesi wanohukumiwa wafanyikazi wa feri hiyo.
Tulikuwa
tumengoja hadi wakati ambapo maji yalianza kuingia kwenye feri
,msimamizi wa darasa alituagiza kuvaa vazi maalum la kuokoa
maisha.mwanahabari wa Reuters aliiga maneno ya mwanafunzi .
''Kupitia
mlango uliokuwa juu yetu tuliweza kuelea na hatimaye tukatoka.wanafunzi
waliotoka mbele yetu walituvuta nje ya meli hiyo.''
Wengi wa Walioaga dunia kwenye meli hiyo ya Sowel walikuwa wanafunzi kutoka shule moja ya upili waliokuwa kwenye ziara ya shule.
Wafanyikazi wanashtumiwa kwa kosa la kutomakinika na kutelekeza majukumu yao .
Nahodha na maafisa watatu pia wanakabiliwa na kosa la mauaji kwa njia ya uzembe kwa makusudi.
Wachunguzi
wanasema kwamba feri hiyo ilikuwa imeundwa kinyume na sheria ili iweze
kubeba abiria na mizigo zaidi,hivyo basi ilikuwa imepitisha kiwango
kinachostahili.
Hata
hivyo waendeshaji mashtaka walisema kuwa tendo la nahodha na wafanyikazi
kuwaagiza abiria kutulia humo ndani feri hiyo ilipokuwa ikizama
kulisababisha vifo zaidi.
Jumatatu ilikuwa siku ya kwanza wanafunzi hao walikuwa wanatoa ushahidi .
Mwanafunzi mwingine alieleza kutoweka kwake kwa kuruka kwenye bahari.
Msichana mmoja alisema kuwa Kulikuwa na wanafunzi wengi katika ukanda wa meli ambao walizuiliwa kwenye feri hiyo.
Mkasa huu
ulisababisha hasira nchini Korea Kusini ikiwemo ukosoaji mkali kwa
wafanyikazi wa serikali na wanabiashara ambao wanasemekana kutowajibika
katika kazi yao ama pia yawezekana ufisadi ulipelekea mkasa huo.
Mwaanzoni mwa mwezi huu,polisi walitambua maiti ya mwenye kampuni inayomilika meli hiyo Yoo Byungeun .
Mwanawe wa kiume Yoo Dae-Kyun alikamatwa ijumaa.Chanzo bbc
No comments:
Post a Comment