Wachezaji wa Argentina wakishangilia ushindi mara baada ya kuifunga Belgium 1- 0 na kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia 2014 baaa ya miaka 24. Picha na Adrian Dennis/AFP/Getty Images.
Wachezaji wa Argentina wakifurahi mara baada ya kupata ushindi uliowawezesha kusonga mbele hatua ya nusu fainali.
Mashabiki mnazi wa timu ya Belgium wakiwa katika sura za uzalendo na nchi yao.
Mchezaji wa Argentina Gonzalo Higuain akiwa na wenzake wakishangilia mara baada ya kuipatia bao timu yake kwa kuifunga Belgium 1 - 0. Picha na Matthias Hangst/Getty
Moja ya pasi nzuri zilizozaa matunda ya ushindi kwa timu ya Argentina. Picha na Julian Finney/Getty Images
Hatimaye Timu ya Argentina imeweza kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Belgiam kwa bao 1 - 0 katika mchezo ulikuwa na msisimko wa hali ya juu.
Bao lililowatoa kidedea Argentina liliweza kufungwa na Gonzalo HiguaĆn dakika ya 8 ya mchezo huo.
Matokeo haya yanaifanya Argentina kusonga mbele huku ikisubiri kuja kumenyana na mshindi ya mchezo wa Netherlands na Costa Rica.
No comments:
Post a Comment