Taswira ya mji wa Mwanga, Moshi
Mshtakiwa
namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB Mwanga
akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu kanda ya
Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika
kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mahakama
imeukataa utetezi wa washtakiwa hao kuwa wakati wa mauaji hawakuwa
nchini, akisema ushahidi wa vinasaba (DNA), umethibitisha walikuwapo
nyumbani kwa mshtakiwa Kanje.
Moshi.
Raia wawili wa Kenya, Samweli Saitoti (Saimoo) na Michael Kimani (Mike),
wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua
polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), PC Michael Milanzi mwaka
2007.
Raia hao
ambao walipambana na polisi jijini Arusha kwa saa sita wakijihami kwa
silaha za kivita yakiwamo mabomu ya kurusha kwa mkono na bunduki aina ya
Sub Machine Gun (SMG), walifanya mauaji hayo yaliyoambatana na uporaji
wa Sh239 milioni mali ya Benki ya NMB, Julai 11, 2007.
Pia, Jaji
Kakusulo Sambo wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, amemhukumu Mtanzania,
Calist Kanje kwenda jela miaka mitano kwa kuwasaidia wauaji hao
wasikamatwe na polisi baada ya kufanya mauaji.
Akitoa
hukumu hiyo jana, Jaji Sambo alisema upande wa mashtaka ukiongozwa na
Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya, Stella Majaliwa na Ignas Mwinuka,
umethibitisha mashtaka hayo pasipo shaka.
Jaji
Sambo alisema ushahidi wa mashahidi 18, umethibitisha kuwa raia hao wa
Kenya ndiyo walioshirikiana kwa pamoja, kumuua polisi huyo ambaye taifa
bado lilikuwa likihitaji utumishi wake.
“Kulikuwa
na hoja ya utetezi kuwa hawakutambuliwa kikamilifu lakini PC Naftali
Ashery aliyekuwa lindo na marehemu aliwatambua vilivyo wauaji hao tena
kwa ukaribu,” alisema. Alisema Mahakama imeridhika kuwa maungamo
waliyoyatoa mbele ya walinzi wa amani ambao ni mahakimu waliyatoa kwa
hiari bila kushurutishwa.
Mahakama
imeukataa utetezi wa washtakiwa hao kuwa wakati wa mauaji hawakuwa
nchini, akisema ushahidi wa vinasaba (DNA), umethibitisha walikuwapo
nyumbani kwa mshtakiwa Kanje.
Jaji
alisema kwa kuwa washtakiwa hao walikwenda kwa Kanje na yeye akawasaidia
wasikamatwe na kuwatorosha, hilo ni kosa la kusaidia wahalifu baada ya
kufanya mauaji.
Jaji
Sambo alisema Kanje ndiye aliyeficha gari aina ya Toyota Land Cruiser
mali ya Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR), lililotumika katika
ujambazi huo na kwamba ushahidi wa wafanyakazi wawili wa mshtakiwa huyo,
unathibitisha kuwa ndiye aliyetoa maelekezo kwa dereva wake ili
akalitelekeze gari hilo eneo la Uwanja wa Ndege wa KIA.
Mahakama
hiyo imeamuru kiasi cha fedha, Dola 8,145 za Marekani na Sh1,769,000
walizokutwa nazo raia hao wa Kenya, zikabidhiwe Benki ya NMB, Mwanga
ziliko
No comments:
Post a Comment