Pages

June 17, 2014

URENO YALA KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA KWA UJERUMANI


Winning with style: The German team come together to celebrate the hat-trick by Thomas Muller (left)

Wachezaji wa Ujerumani wakumpongeza mwenzao Thomas Muller (kushoto) baada ya kupiga hat-trick leo.
MJERUMANI Thomas Muller awa mchezaji wa kwanza  kufunga mabao matatu katika mechi moja `hat-trick`  kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil baada ya kuiongoza nchi yake kuilaza Ureno mabao 4-0 usiku huu mjini Salvador.
Nyota huyo wa Bayern Munich alifunga bao la kuongoza dakika za mapema kwa mkwaju wa penati na kuwapa mwanzo mzuri katika uwanja wa Arena Fonte Nova wana nusu fainali hao wa mwaka 2010 nchini Afrika kusini. Mabao ya Muller usiku huu yalifungwa katika dakika za  12 (penati), 45, 78, na goli lingine lilifungwa na beki wa kati Mats Hummels katika dakika 32
Ureno walipata majanga baada ya mshambuliaji wake wa kati Hugo Almeida na Fabio Coentrao kupata majeruhi, lakini mbaya zaidi walishuhudia  beki wao wa kati Pepe  akitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati timu yake iko nyuma kwa mabao 2-0 baada ya kumfanyiwa madhambi Muller.
Poaching: Muller turns the ball in from three yards to complete his hat-trick  Muller akifunga bao la tatu na kukamilisha hat-trick
Net gains: MUller goes to ground as the ball trickles past Eduardo in the Portugal goal
Manyoya tu: Muller akimtungua kipa wa Ureno  Eduardo
Hapa chini ni vikosi vya timu zote mbili na viwango vyao katika mchezo wa leo. Alama ni juu ya kumi.
 Kikos cha Germany: Neuer 6; Boateng 6, Mertesacker 6, Hummels 7 (Mustafi 73min, 6), Howedes 6, Lahm 7; Khedira 7.5, Kroos 6; Muller 8 (Podolski 80), Ozil 5.5 (Schurrle 63, 6.5), Gotze 7.
Wachezaji wa akiba: Zieler, Grosskreutz, Ginter, Schweinsteiger, Klose, Draxler, Durm, Kramer, Weidenfeller.
 Magoli: Muller 12 (pen), 45, 78, Hummels 32
Kikosi cha Ureno: Patricio 5.5; Pereira 5, Alves 5, Pepe 2, Coentrao 4.5 (A Almeida 65, 5.5);  Moutinho 5, Veloso 5 (Costa 45, 5), Meireles 5; Nani 6, H Almeida 5 (Eder 23, 5), Ronaldo 5. 
Wachezaji wa akiba: Eduardo, William Carvalho, Vieirinha, Luis Neto, Rafa, Varela, Ruben Amorim, Postiga, Beto.
Kadi ya njano: Pereira.
Kadi nyekundu: Pepe.
Mchezaji bora wa mechi: Thomas Muller.
Mwamuzi: Milorad Mazic (Serbia)

Isolated: Ronaldo cuts a frustrated figure as Portugal collapse in the first half
 Ronaldo ameachwa hoi baada ya kupigo cha leo
Keeping him out: Hummels (right) goes to block a Ronaldo shot on goal
 Hummels (kulia) akizuia shuti la Ronaldo lililokuwa linakwenda nyavuni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...