Ndosi hiyo!: Robin van Persie akifunga goli kwa kupiga kichwa matata na kuisawazishia Uholanzi.
Kosa kubwa la mlinda mlango: Van Persie akimpoka Iker Casillas mpira na kufunga bao la nne.
Haamini: Casillas akitafakari baada ya kufungisha bao la nne, huku wachezaji wa Uholanzi wakishingilia bao hilo la Van Persie
Vikosi na viwango vya wachezaji katika mchezo wa leo kwa mujibu wa Joe Callaghan ambaye yupo mjini Sao Paulo. Alama zilizotumika ni 10.
Kikosi cha Hispania: Casillas 5, Azpilicueta 6.5, Sergio Ramos 5.5, Pique 5.5, Jordi Alba 7, Alonso 7.5 (Pedro 63), Xavi 7, Busquets 6, Silva 7.5, Diego Costa 7 (Torres 62), Iniesta 7.
Wachezaji wa Akiba: De Gea, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Villa, Fabregas, Mata, Koke, Cazorla, Reina.
Kikosi cha Uholanzi: Cillessen 7, Janmaat 6, Vlaar 7.5, De Vrij 7, Martins Indi 6.5, Blind 7, de Guzman 6, Sneijder 6, De Jong 6.5, Van Persie 8, Robben 8.
Wachezaji wa akiba: Vorm, Verhaegh, Veltman, Kongolo, Kuyt, Clasie, Lens, Fer, Huntelaar, Wijnaldum, Depay, Krul.
Mwamuzi: Nicola Rizzoli (Italia)
Mchezaji bora wa mechi: Robin van Persie na Arjen Robben
Mabao yote ya Uholanzi yalikuwa ya ajabu. Yote yalitengenezwa kwa pasi murua kutoka wingi ya kushoto kutokea kwa Daley Blind na pasi zilimaliziwa kwa ufundi tofauti na wachezaji Robin van Persie na Arjen Robben.
Magoli manne yalitokana na makosa ya mlinda mlango Iker Casillas. Kuelekea mechi ijayo itakayochezwa wiki ijayo ambayo Hispania wanahitaji ushindi- kuna hoja kuwa kipa wa Manchester United, David de Gea anaweza kumbadili mlinda mlango huyo mkubwa wa Hispania.
Bao la tano: Robben (kushoto) akiifungia Uholanzi bao la tano.
Stefan de Vrij (kushoto) akiifungia Uholanzi bao la tatu.
Hapa anageuzwa: Arjen Robben akimpiga chenga Gerard Pique
Iker Casillas (kulia) alipelekwa sokoni
Fungeni midomo: Diego Costa akiwanyooshea kidole mashabiki wa Salvador ambao walimzomea dakika zote alipokuwa uwanjani.
Costa aliangushwa na Stefan de Vrij na mwamuzi kuamuru mkwaju wa penati
Xabi Alonso alifunga penati hiyo
No comments:
Post a Comment