Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi ( wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo mchana
UCHAGUZI
wa Simba sc kwa asilimia kubwa utaweza kufanyika juni 29 kama
ilivyopangwa kufuatia kauli ya Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF,
Jamal Emil Malinzi akimpongeza rais wa Simba Ismail Aden Rage kwa
kufanya juhudi ya kufanya mazungumzo na shirikisho hilo.
Akuzungumza
mchana huu na waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho hilo
zilizopo katikati ya jiji, Posta, Rais Malinzi amesema tangu
alipotangaza kusimamisha uchaguzi huo jumapili iliyopita na kuwataka
Simba kuunda kamati ya maadili itakayosikiliza masuala yao ya maadili,
rais wa Simba, Aden Rage amekuwa akiwasiliana naye vizuri na kwa heshima
ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Malinzi alisema wamekuwa na maelewano mazuri na Rage, hivyo ana imani ufumbuzi utapatikana .
Maneno ya Malinzi yanatoa imani kuwa yeye na Rage wameshafikia hatua nzuri na bila shaka uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa.
“Nimpongeze
sana mwenyekiti wa klabu ya Simba pamoja na kamati yake ya utendaji,
kuanzia siku ya jumapili hadi leo hii tumekuwa tukiwasiliana kwa karibu
sana, katika hali ya maelewano, heshima kubwa”. Alisema Malinzi mchana
huu.
“Na
niseme tu kwamba leo mgombea mmoja ambaye kamati ya uchaguzi ilimuondoa
katika uchaguzi, sina haja ya kutaja majina hapa, alileta rufaa
yake, leo saa nane mchana kamati ya rufaa inakaa”. Aliongeza Malinzi.
Malinzi
alisisitiza kuwa baada ya zoezi la leo la kusikiliza rufaa kukamilika,
mazungumzo yataendelea baina ya TFF na Simba kwa ajili ya ustawi wa soka
la nchi hii.
“Baada
ya hapo, vyovyote vile itakavyokuwa baada ya zoezi ya leo, mazungumzo
yataendelea baina ya TFF na klabu ya Simba, ni imani yetu kwamba kwa
ajili ya ustawi wa mpira wa nchi hii, kwa maana yoyote ile, tunaamini
ufumbuzi utapatikana”.
“Sasa
ni ufumbuzi gani utapatikana, siwezi kuuzungumzia sasa hivi, mimi
nimeruhusu kwa maana ya shirikisho kwamba kikao kifanyike leo cha kamati
ya rufaa ya uchaguzi”.
“Na
baada ya hapo, mazungumzo yataendelea kuweza kuona ni kwa namna gani
tutaweza kuwa katika hali nzuri ambayo itaweza kuwasaidia ndugu zetu wa
Simba wakaendeleza ustawi wa klabu yao”. Alisema Malinzi”.
Mgombea
aliyeenguliwa kwa mara ya pili na kamati ya uchaguzi wa Simba chini ya
mwenyekiti wake, Wakili Damas Daniel Ndumbaro, Bwana Michael Richard
Wambura amekata rufaa kupinga maamuzi hayo kwa mara nyingine.
Kamati
ya Ndumbaro ilimuondoa tena Wambura kwa madai kuwa baada ya kurudishwa
katika uchaguzi na kamati ya rufani ya TFF chini ya mwenyekiti wake,
Wakili Julius Mutabazi Lugaziya aliongea maneno ambayo ni kampeni kwenye
vyombo vya habari wakati zoezi la kampeni bado halijaanza.
No comments:
Post a Comment