Siku
chache baada ya kutoa wosia kuwa akifa asizikwe kwa mbwembwe, mwigizaji
Devotha Mbaga amezimia ghafla wakati wa kuaga mwili wa mwongozaji wa
filamu na vipindi mbalimbali Bongo, marehemu George Otieno ‘Tyson’.
Kwa
mujibu wa chanzo kilichoomba kusitiriwa jina (msanii), baada ya mwili
wa Tyson kuagwa katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu,
ghafla Devotha alikutwa amezimia kwenye gari lake.
alisema msanii huyo.
Baada
ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walifika katika Zahanati ya
Mico alipokuwa amelazwa na kumkuta msanii huyo akiwa amewekewa dripu
huku akizungumza kwa shida akidai hakujua kilichoendelea mpaka
aliposhtuka akiwa kitandani hospitalini hapo.
alisema Devotha.
Kwa
upande wake msanii Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ ambaye alikuwa
hospitalini hapo alisema, inawezekana sababu ya Devotha kupandwa na
presha kiasi hicho ni kutokana na vifo vya wasanii vilivyotokea
mfululizo.
alisema Bi Mwenda.
Katika
moja ya machapisho yetu mwanzoni mwa wiki Devotha alikaririwa kuwa
endapo atafariki, hahitaji mbwembwe za kununuliwa vitu vingi vya gharama
kama jeneza katika maziko yake, badala yake akashauri fedha hizo bora
wapewe wanawe atakaowaacha duniani.
No comments:
Post a Comment