.Mkuu
wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akipokea maandamano ya
wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya mazingira
jijini Dar es salaam.Kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
Kikundi
cha ngoma za asili kutoka shule ya msingi Umoja kikitoa burudani wakati
wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika katika uwanja wa
Mnazimmoja jijini Dar es salaam.Baadhi
ya wananchi na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jiji la Dar es
salaam wakiwa kwenye maandamano huku wakiwa wamebeba mabango yenye
ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha wiki ya mazingira duiniani leo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
………………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.Dar es salaam.
Serikali
mkoa wa Dar es salaam imewataka watendaji wote wenye dhamana ya
uhifadhi wa mazingira kulinda na kusimamia usafi na utunzaji wa
mazingira katika maeneo mbalimbali ya jiji ili kufikia malengo ya kuwa
na jiji safi na salama.
Mkuu
wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akizungumza kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa suala la utunzaji
wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi na kusisitiza kuwa watendaji
katika mamlaka mbalimbali za jiji la Dar es salaam wanalojukumu la
kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria zilizowekwa.
Amesema
Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha kilele cha
wiki ya mazingira duniani kwa mwaka 2014 kwa ngazi ya mkoa na taifa kwa
kueleza hatua zilizofikiwa katika uhifadhi wa mazingira na kueleza kuwa
kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Mwanza chini ya Kauli Mbiu
Tunza Mazingira ili Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Amesema
uongozi wa mkoa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha
jiji la Dar es salaam linakuwa safi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa
sheria ndogo zinazohusiana na usafi na utunzaji wa mazingira kwa
kuwabana wanaochafua mazingira kwa kutupa ovyo,utiririshaji wa majitaka
kwenye mitaro ya barabara, kuzuia uchimbaji wa mchanga,Vifusi na kokoto
katika kingo za mito na maeneo yote yasiyo rasmi.
Hatua nyingine ni kudhibiti ujenzi holela katika maeneo yanayozuia mikondo ya maji mabondeni na kuzuia ufanyaji wa biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Hatua nyingine ni kudhibiti ujenzi holela katika maeneo yanayozuia mikondo ya maji mabondeni na kuzuia ufanyaji wa biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Bi.
Mjema ameeleza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea sasa
yanasababisha ongezeko la joto duniani,kuongezeka kwa kina cha bahari na
kusababisha kumomonyoka na kuzama kwa fukwe za bahari,ongezeko la
vipindi virefu vya ukame, ongezeko la mvua nyingi zaidi ya viwango vya
kawaida hali inayosababisha mafuriko na kuambatana na milipuko ya
magonjwa mbalimbali.
Kuhusu
kauli mbiu ya mwaka huu amesema kuwa inatoa chagizo kwa wananchi
kuanzia mtu mmojammoja kutoa mchango katika kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi na kutoa wito kwa jamii kutathmini madhara
yatokanayo ya shughuli za kibinadamu zinazoongeza hewa ya ukaa zikiwemo
za uchomaji wa mkaa, misitu, moshi kutoka viwandani na kwenye magari na
baadhi ya vifaa vya majumbani kama vile majokofu na viyoyozi.
“Mabadiliko
ya tabia nchi yana athari kubwa sana katika mazingira yetu, wataalam
wanatuambia kwamba njia ya asili ya kupunguza hewa ukaa angani ni kuwa
na misitu,nasisitiza tuwe na utamaduni wa kupanda, kutunza na kuhifadhi
misitu yetu kwani hunyonya hewa hiyo, hii ni sababu mojawapo
inayonifanya kusisitiza suala la kupanda na kutunza miti” Amesema.
Aidha,
ameeleza kuwa maadhimisho ya wiki ya mazingira mkoa wa Dar es salaam
yalitanguliwa na shughuli mbalimbali zinazohamasisha utunzaji na
usimamizi wa mazingira katika halmashauri za manispaa ya Kinondoni,
Ilala na Temeke kuanzia tarehe 1 mpaka tarehe 5 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment